RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

POLISI WAMTAFUTA MCH. GWAJIMA BILA MAFANIKIO


Polisi jana walipiga kambi kwa saa saba kwenye geti la nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wakitaka kumkamata bila ya mafanikio. 

Polisi hao walikuwa kama wageni wa askofu huyo wakisubiri wafunguliwe geti, kuanziasaa 3:00 asubuhi hadi saa 10:10 jioni walipoamua kuondoka wakitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye namba za kiraia, ambalo kwa muda wote huo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa geti hilo.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha takriban miezi 16, kwa askari wa jeshi hilo kwenda nyumbani kwa askofu huyo na kushinda mbele ya nyumba yake kwa saa kadhaa, kabla ya kuondoka bila ya kumtia nguvuni.

Tukio hilo pia linatokea wakati kukiwa kumesambaa mkanda unaotoa sauti ya Askofu Gwajima, ikizungumzia kitendo chake cha kuamua kumuunga mkono Rais John Magufuli na kumshutumu Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ikiitaka afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo Rais wa sasa anayashughulikia.

Jana, mbele na nyuma ya gari hilo kulikuwa na askari waliokuwa wamevalia kiraia, kila mmoja akionekana kama anafanya shughuli tofauti, lakini wote wakionekana kuwa na lengo moja; kusubiri kufunguliwa lango la nyumba ya Askofu Gwajima.

Mbele ya nyumba walikuwapo askari watatu na raia wawili, mmoja mwanamke na mwingine mwanamume ambao baadaye ilibainika kuwa walikuwa wamezuiwa na askari hao baada ya kuonekana wakitokea mlango wa nyuma wa nyumba hiyo.

Mwandishi alishuhudia mwanamke huyo akiitwa na askari aliyekuwa ndani ya gari na kuonywa kuepuka kutumika, kisha akarudishiwa simu yake ambayo walikuwa wakiishikilia.

Raia hao walisema, walifika kwenye nyumba hiyo kwa ajili ya kufanya tathmini ya matengenezo na baada ya kumaliza walipokuwa wanatoka wakakutana na askari hao na kukamatwa.

Askari hao wasikika wakisemezana kuwa kuna taarifa zinasambazwa kwenye simu kuwa nyumba ya kiongozi huyo wa kiroho, ambaye aliibuka kuwa maarufu mwishoni mwa mchakato wa Katiba Mpya, imezingirwa, wakati hakukuwa na kitu kama hicho.

Pia, askari hao walisikika wakieleza kushangazwa na kitendo cha wenyeji kutowafungulia geti hilo ili waingine.