RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RONALDO NA MESSI NDIO WANASOKA PEKEE WALIOINGIA KATIKA TOP 10 YA WANAMICHEZO MATAJIRI DUNIANI

Forbes wametoa list ya wanamichezo 100 matajiri duniani, kwa upande wa TOP 10 mchezo wa soka ambao ndio unatazamiwa kuwa unaingiza hela nyingi, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi pekee ndio wamefanikiwa kuwa na utajiri uliowafaya waingie TOP 10.

Top 10 ya wanamichezo matajiri duniani

Ronaldo ndio ameongoza katika list ya wanamichezo matajiri duniani kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 88 ambazo ni zaidi ya bilioni 190 za kitanzania, Lionel Messi ameshika nafasi ya pili kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 81.4 ambazo ni zaidi ya bilioni 178 za kitanzania.

Cristiano Ronaldo utajiri wake wa dola milioni 32 ambazo ni zaidi ya bilioni 70 za kitanzania unatokana na mikataba ya matangaza kupitia account zake za social network kama twitter, instagram na facebook.