RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TUNAKUPONGEZA WEWE ULIYEOKOKA SIKU YA JUMAPILI 19.06.2016 KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kukupongeza wewe uliyeamua kuokoka siku ya Jumapili 19.06.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" linaloongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Uamuzi wako ni sahihi kabisa na una kila sababu ya kumshukuru Mungu wako kwa kukuongoza na kukutia moyo katika maamuzi magumu na yenye faida ya kumtumikia Mungu.

Wapo watu wengi sana wanapitia taabu na wengine wanakula raha za dunia lakini hawajabahatika kupata maono hayo ambayo umeyapata kupitia Roho Mtakatifu. Wengine wanatamani kuokoka lakini kuna nguvu fulani imewakaba na hawana msaada wowote, lakini wewe ulijinasua kat0ika mtego huo na sasa uko huru kabisa.

Sasa umeanza maisha mapya, na katika safari hii kuna mlima wa mabonde, na yakupasa kusafiri na kupitia hayo yote ili ufike kule unakotaka kufiika, Imani yako na ujasiri wako ndio utakaokufikisha mbinguni na sio mtu anaweza kukufikisha mbinguni. Huu ni muda wako mzuri wa kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu na pia kuwa karibu sana na watumishi wa Mungu kwa kufuata yale wanayokufundisha kwani wao ni chombo cha Mungu.

Unahitaji kusoma sana Neno la Mungu na kuyafuata yale unasoma katika Biblia yako. Kila unachosoma katika Biblia yakupasa kukifanyia kazi ili kiweze kuleta matunda katika maisha yao.

Simama imara kwa kuwaleta watu klwa Yesu kwa njia ambayo Mungu atakuambia uitumie. Yawezekana ikawa kwa njia ya uimba, misaada, kuhubiri, kuandika habari njema katika mitandao, kushuhudia, kusambaza kazi za Mungu, kuwatia moyo wenye uhitaji wa faraja, kutangaza radioni au katika TV, kucheza, kuingiza n.k.

Muombe sana Mungu akupe kitu cha kufanya katika kazi yake. Usikae kanisani ukawa ni mtu wa kupokea tu kutoka madhabahuni, jishughulishe ili Mungu akuinue na kukubariki katika kazi yako. Mungu na akubariki sana na uzidi kuhudhuria ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B"







BAADA YA KUONGOZWA SALA YA TOBA NA KUOMBEWA WALIPELEKWA BAHARINI KUBATIZWA