RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ULIPOFIKIA MPANGO WA AFRIKA KUTUMIA PASSPORT MOJA KWA NCHI ZAKE ZOTE

Kila nchi duniani huwa na Passport kwa ajili ya raia wake kuweza kusafiri katika nchi za watu kirahisi, viongozi wa umoja wa nchi za Afrika kwenye vikao vyake umepanga kutambulisha matumizi ya passport moja tu itakayotumika katika nchi zote za Afrika ili kurahisisha safari za ndani ya Afrika.


Wazo hili limezaliwa ndani ya ule mfumo huru wa safari za ndani ya bara la Ulayaambapo nchi zake zote hufanya safari bila visa ndani ya bara hilo. Mpaka sasa nchi 13 za Afrika zina mikataba ya safari za bila visa kwa nchi nyingine za ndani yaAfrika, ambapo raia wake usafiri bila ya visa ama kupokea visa wanapowasili.

Viongozi wa nchi za Afrika watakapokutana Kigali Rwanda July 2016 watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutumia passport hizo za kielektroniki. Lengo ni kurahisisha safari za ndani ya Afrika na inaaminika pia biashara za ndani zitaimarika na kukuza uchumi kwa ujumla pia kuimarisha ujamaa na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo.