MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

VIDEO: VURUGU ZA WAINGEREZA NA WARUSI KOMBE LA EURO 2016 USIOMBE YAKUKUTE

Waziri wa maswala ya ndani wa ufaransa , Bernard Cazeneuve, ametoa ushauri kwa wakuu wa miji mbalimbali wenyeji wa kinyanganyiro cha soka barani ulaya Euro2016, kupiga marufuku matumizi ya pombe katika maeneo tete siku ya na hata kabla ya siku ya mechi kufanyika.

Hii ni kutokana na matukio ya wafuasi wa timu kadhaa kushambuliana katika visa vilivyochochewa na ulevi huko mjini Marseille katika kipindi cha siku 3 zilizopita.

Shirikisho la kandanda barani ulaya , UEFA, limeonya kuzichukulia hatua ya hata kuwafurusha kutoka mashindano hayo timu za Uingereza na Urusi iwapo mashabiki wao watajihusisha tena na matukio ya ghasia kama ilivyotokea wakati wa mechi yao katika mji wa Marseille .

Ulevi unatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo ambapo baadhi ya mashabiki wana kwenda katika viwanja vya michezo wakiwa wamelewa chopi.

Serikali ya Uingereza tayari imeahidi kutuma idadi kubwa ya maaskari wa kupambana na fujo kabla ya mechi ijayo inayohusisha timu ya Uingereza siku ya Alhamisi.

Bwana Cazeneuve amenukuliwa akisema

”Tutafanya kila tuwezalo kuzuia ghasia na machafuko zaidi ikiwemo kuzuia uuzaji wa pombe unywaji wa pombe na hata usafirishaji wa pombe kuelekea maneo wenyeji wa kombe la Euro”

”Tutaweka marufuku ya pombe katika maeneo yote ya umma”

Vilevile baa na migahawa inayouza tembo italazimika kubadilisha mikebe na chupa wanayouzia pombe ilikuzuia madhara yanayotokana na walevi kutumia vyombo hivyo kama makombora haswa dhidi ya polisi”

alisema bwana Cazeneuve.

Mwenyekiti wa chama cha mpira cha Uingereza, Greg Dyke amewaandikia barua chama cha shirikisho la soka barani Ulaya,UEFA kutoa maelezo ya tija kuhusu mpangilio wa ulinzi wakati wa michuano ya soka ya Euro 2016.

Leo Urusi itacheza katika mji wa Lile ambapo mashabiki wa Uingereza pia watakusanyika hapo kwa kuwa mechi yao itakuwa kesho. Kulikuwa na usumbufu mkubwa katikati hapo wakati timu zote zilipopangwa mwishoni mwa juma. Mashabiki sita wa England wamefungwa kutokana na vurugu zilizotokea lakini hakuna yeyote kati ya mamia ya mashabiki wa Urusi aliyewekwa hatiani,Maafisa wa Ufaransa wameliita tukio hilo kuwa ni vurugu za kihuni,hivyo timu zote mbili zilipaswa kutolewa katika michuano kama patatokea vurugu nyingine.

Shirikisho la kandanda barani ulaya , UEFA, limeonya kuzichukulia hatua na hata kuzifukuza timu za Uingereza na Urussi.

Hatua hiyo ni kufuatia mashabiki wa timu kuwa chanzo cha ghasia zinatokea kama ilivyotokea wakati wa mechi yao ya huko Marseille.

Suala la ulevi linatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo ambapo baadhi ya mashabiki wana kwenda katika viwanja vya michezo hiyo huku wakiwa wamelewa.