RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

10.07.2016: KWAYA JOYBRINGERRS NA HAPPY KWAYA ZAFANYIKA BARAKA KWA WAAMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTOMIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kwaya ya Joybringers na Happy Kwaya kwa kazi ya Bwana waliyoifanya siku ya Jumapili. Kwaya hizi zote ni za Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Mungu ameweka hazina ndani ya hawa waimbaji, wamefanyika chombo cha Mungu kwa wanadamu kupitia uimbaji wao. Nyimbo zao zimekuwa na mguso wa kipekee sana. 
Mama Kibona

Siku ya Jumapili 10.07.2016 kwaya hizi zilikonga mioyo ya watu na kuwaweka katika uwepo wa Mungu. Wapo waliweza hata kutoa machozi wakilia kutoka na jinsi walivyoguswa na uimbaji wao. Na pia kanisa lilibarikiwa sana kumuona Mama Kibona akiwa ameungana na kwaya akiimba baada ya kurudi kutoka India kwenye matibabu. 
Watu walimiminika madhabahuni kumfariji Mama Kibona ambaye ni kiongozi wa moja ya hizo kwaya mbili, na wengine kutoa sadaka zao kwaajili ya kuwapongeza waimbaji hawa. Tuna kila sababu ya kuwaombea ili wazidi kudumu katika Bwana. 
Tuwaombee wakabarikiwe katika kazi zao za mikono, wasio na kazi wakapate kazi, wasiooa au kuolewa wakaolewe na kuoa, wenye uhitaji wa watoto wakapate watoto, wanaosoma wakafaulu, wagonjwa wakapone, na kila wanachokihitaji kikafanikiwe katika jina la Yesu Kristo.
Tunakukaribisha wewe ambaye hukufika katika ibada hii ya Kufunguliwa Kwako. Jumapili hii ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha Makumbusho cha mabasi au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Mungu akuwezeshe kufika kanisani Jumapili hii