MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

28.06.2016: BISHOP DANSTAN MABOYA AHUBIRI UJUMBE MZITO KATIKA SEMINA YA MID-CROSSOVER MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JUU YA MANABII FEKI, KUTOTUMIA NYOTA NA WATU KUJENGA NYUMBA ZA KUISHI NA SIO KUPANGA


Bishop Danstan Maboya siku ya Jumanne 28.06.2016 katika semina ya Mid-Crossover iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” aliweza kufundisha mengi na mojawapo ni Utoaji wa Fungu la Kumi, Chanzo cha watu waliokoka na mwisho aliwaonya watu wanaoishi nyumba za kupanga. Tukianza na CHANZO CHA ULOKOLE alisema


“Ninaomba ukalie kiti chako cha muujiza. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alipokuwa akihubiri juu ya Mbweha Wadogowadogo nikaona sasa tuombee wagonjwa na tukusanye sadaka, maana ujumbe wote umekamilika. Naomba usome Ayubu 12:12. Ukiona mpaka Mungu anasema wazee ndio wenye hekima

Leo hii kuna neema kubwa kwa maana Injili tunayoiona leo haikuweko miaka ya 70. Kuna watu wameteseka sana kwaajili ya uamusho huu unaoneka hivi leo hapa nchini. Miaka ya 70 mwanzo au miaka ya 60 mwishoni kulikuwepo makanisa machache sana ya Kiroho. Ninakumbuka kwa wale waliokuwepo upande wa Assemblies ilikuwa Temeke, Ilala na Kinondoni na kupitia hayo yakawa yamejaa kila sehemu, na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa Ilala. Unapoona makanisa yamepanuka hivi ujue kilindi chake kilikuwa ni Lindi Street hapa jijini Dar es Salaam, nguvu ilikuwa inatoka Temeke, Ilala na Kindoni, watu waliishi kama ndugu.

Kipindi hicho kulikuwa na tatizo kubwa sana la pesa, mkimpata mfadhili kama meneja mnamuona ni kama Roho Mtakatifu. Hali ilikuwa ni ngumu sana, hata wasomi, ma-“Lecture” walikuwa ni wachache wanaomjua Mungu. Hao ma-“Lecture” waliokoka na kumjua Mungu ni wale waliokoka miaka ya 70 mwishoni au miaka ya 80 mwanzoni. Kipindi hicho Injili tulikuwa tunaimba “Mlima Yote na Mabonde Injili ya Yesu Itasimama”. 
Mtu anapigwa lakini bado ana nena, watu wanatembea na nguo aina moja. Injili iliwekwa kwenye misingi mikali mno, lakini ninashikuru Mungu kwaajili ya mtumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude RwakatareWalolokole walipewa angalizo, walokole wa kwenda Marekani walikuwa ni wachache mno, na wengine wakiona mtu amekwenda Marekani wanasema ametoroka huduma. Lakini Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kwenda marekani na aliporudi akili yake ikapevuka, na akili ilipopevuka akaja na ufahamu huu wa Ujasiriamali. 

Nakumbuka hapo zamani mtu aliyeokoka anapigwa lakini bado ana nena, watu wanatembea na nguo aina moja. Injili iliwekwa kwenye misingi mikali mno, lakini ninashukuru Mungu kwaajili ya mtumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Walokole walipewa angalizo, walokole wa kwenda Marekani walikuwa ni wachache mno, na wengine wakiona mtu amekwenda Marekani wanasema ametoroka huduma. Lakini Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kwenda marekani na aliporudi akili yake ikapevuka, na akili ilipopevuka akaja na ufahamu huu wa Ujasiriamali. 

Ninasema sitakosea nikisema katika wajasiriamali wa kwanza kwenye makanisa ya Kilokole hapa Tanzania ni mama Gertrude Rwakatare. Kanisa hili kubwa unaloliona msingi wake ulikuwa ni shule ya msingi, alikuwa anatembea nyumba kwa nyumba akiwahubiria watu habari njema. Unajua siku zote msingi haupigwi rangi. 
Kwenye nyumba kinachopendeza ni ukuta na vigae lakini vyote vinavyopendeza vimejengwa kwenye msingi wa mawe ambao ni mchafu. Na kama uzuri wa juu (vigae na dali) hauna msingi basi nyumba haitasimama. Na ndio maana Wameru kule Arusha wanausemi mmoja, “Ukiangalia miguu ya mkamua maziwa hutakunywa kilichobebwa” Ukitaka kunywa maziwa usiangalie miguu ya mkamuaji. Ukiangalia yale maziwa ujue yale yametoka kwenye zizi, na huwezi kuyapata lazima upigwe na baridi. Wakamuaji mara nyingi huamka saa 11 alfajiri kukamua maziwa.

Hivi sasa uamusho ni mkubwa kwasababu msingi ulishawekwa, wameinuka watu wa kila namna na hata wenyewe hawalewi wamelipa gharama zipi. Sasa leo unaona watu wanaumba maneno laini, wakiomba hiki na hiki, nasema, “Usisahau Ulikotoka” kwasababu huko ulikotoka kutakusaidia.

Kipindi cha nyuma wahubiri wote wakitaka kusafiri kwenda mikoani walikuwa wanakwenda kwa Mama Manda Railway. Mtu huyu amewakatia mizigo wachungaji wote Afrika Mashariki wanaokwenda mikoani, amewasaidia sana.

Ninachotaka kusema ni kwamba ndani ya wazee iko hekima, iko busara. Na shetani anakuja kwa hali ya juu sana, shetani anachokifanya sasa, anakung’oa katikati ya watu wenye busara halafu anawakeka kwa mavuvuzera wanaopiga kelele ambao hawawezi kukupa ushauri wa kimaisha. Watu wanakemea mapepo lakini hayaitiki, mpaka yanakuuliza, “Wewe unamjua Yesu?”, kwasababu hujui maandiko, utakung’utwa makofi.

Leo hii imefika kipindi watu wanapeana unabii wa kutishana, na wengine wanafika kipindi wanatabiri vitu ambavyo havipo, na wengine wanaenda mbali zaidi, wanatumia nyota, wamesoma vitabu vya “Napoleon” kwa kujua tabia za watu. Sisi kama watumishi wa Mungu tunaelewa kuwa ngoma hii sio sawa kwasababu tunaongozwa na Jehova.

Kuna watumishi wanamwenendo wa kinabii na wengine kufariji na wengine wa kutia moyo, hivi ni vitu tofauti, mtu anakuja kujua maisha yako na kuanza kukutabiri uongo. Kuna wahubiri wengi hawaishi sawasawa na mahubiri waliyonayo. Utakuta wana mahubiri mazuri lakini maisha yao ovyo, Neno zuri lakini nyumba yao kama gesti, neno zuri lakini meseji yake ina mameseji ya ovyo. 

Na wapo ambao wanachukua mahubiri yao kwenye “Internet” na kurekodi mahubiri ya watu wengine na wanakula dili na wenyeji na kuanza kutoa unabii feki. Lakini wakati umefika watu kujua kweli ya Mungu na kuokolewa kutoka kwa hawa manabii.

Kazi kubwa ya leo ya wana huduma ni kusema ukweli, watu wanadanganywa, wewe unakwenda kichwakichwa kwa Nabii kumbe amekuchora kila kitu. Na ndio maana kabla hujaenda hata kama ni uani au chumba cha mtu, mshirikishe mkufunzi kwa kuwa Mungu hajasema “Usikilize sauti ya Nabii, bali Sikiliza sauti ya Mchungaji wako” Ila Nabii unamwamini ila humsiikilizi. Kuna utofauti wa kumwamini maana yake unakuwa “gentle” kwake, unasikia ile meseje kutoka kwa Nabii na unaipeleka kwa mchungaji nay eye anaitafsiri. Na ndio maana Nabii zote ulizopewa haijatimia hata moja kwasababu ya kugonganisha. 

Kuna watu ambao wamesomasoma kidogo, lakini sisi ambao tuliwahi kuingia shule tukachelewa kusoma, inasumbua kidogo. Ila kuna wale ambao wamesomasoma kidogo na wameenda viwanja na wanajua kusema, “How are You”. Kuna watumishi wengine wanajua kutabiria majina ya watu, akijua wewe ni Otieno wanachambua jina lako na wanakutafsiri kama lilivyo na wanakupa jibu la maisha yako. 
Wengine wanatumia nyota, kama unavyoona kwenye magazeti, kuna nyota ya simba, nge, mapacha, samaki n.k, nao wanakuwa wamesoma elimu au nyota za magharibi na kuna ambao wamesoma nyota za Kichina na wakipata mwaka wako tu wakuzaliwa wanajua jinsi ulivyo. Na kuna wale ambao wanajua nyota za Kiarabu, wanachukua jina lako na la mama yako, akigawanya anajua jinsi ulivyo. Na ndio maana Yesu anasema, “Mtu akiwa ndani ya Yesu Kristo, tazama ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya”. 

Ukienda nchi za mbali, ukitembea tu tayari ameshakujua. Hata kwenye ukoo utakuta mama anapandisha kiti juu chini juu chini na mizimu yake ukajua ni kweli, kumbe anacheza na akili yako. Ninakuambia issue ni kutatua matatizo uliyonayo na sio kukutabilia tu na anakuacha hapo ulipo . Ukiniambia nina tatizo nasema, “Sawa, ila ninachotaka mzigo (tatizo) utoke”. 
Mtu nayeweza kutoa mzigo (tatizo) ni Kristo peke yake. Kristo amejieleza vizuri kwenye Ufunuo 22:16, inasema “Mimi Yesu nimetuma Malaika wangu kuwashuhudia watu mambo hayo katika kanisa, mimi ndiye niliyeshina na mzao wa Daudi ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi” Hii ndio nyota tunayoiitaji sisi, na sio nyota kutoka India, Marekani au China tunatakiwa kuongozwa na nyota ya Daudi abayo inatakiwa kuingia kwetu na kufanya kazi..

Ngoja nikueleze ujinga wa walokole wanaotumia kwenye mambo ya nyota na kutabiri. Nisomee Isaya 47:12-13 inasema, “Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako uliojitaabisha sana tangu ya ujana, labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushida, umeschoka kwa wingi kwa mashauri yako. Muokoe na mambo yatakayompeta.” Unajua waganga wa kienyeji, wachawi wanatabiri uongo. Ninyi mnaokwenda kwenye mambo ya nyota, eti nyota yangu samaki, nge n.k, kuanzia leo iteme hiyo nyota. Kuanzia sasa tuna nyota ya asubuhi inayotoka kwa Baba, na kupitia hii utapata faida. 

Waganga wa kienyeji wanatabiri. Kuna jamaa yangu alikuwa anatokea misheni, mara akatokea kijana anajifanya kilema wa mguu anaomba msaada, Yule jamaa akamwangalia na akapuuzia kumsaidia, akatokea mtu mwingine akamwambia Yule jamaa, naomba umsaidie, tumpeleke hapo Mwenge mara moja akatibiwe. Yule jamaa akakupalia na Yule mtu kumpeleka huyu mlemavu hospitalini, na walipo fika mbele Yule mtu akasema, “Sasa naomba tumfanyie maombi kwasababu mimi huwa na nafanya na watumishi wa Mungu” Walipofanya maombi akaomba jina la Baba yake Yule jamaa na alipompa tu jina, Yule mtu akamtabiria kuwa utakufa tarehe Fulani. Jamaa baada ya kupokea utabiri huo akanipigia simu, nikamwambie amwambie, “Ashindwe kwa Jina la Yesu”.
 Watu wanacheza na nyota za watu . Mimi ninakuambiwa ukitabiria na mtu yeyote au mganga usiyashike bali sikiliza sauti ya mchungaji wako.Ukiona Nabii amekuja kwako na anakueleza mambo yako yote ya ndani yasikilize vizuri yawezekana kapewa taarifa zako na sio Mungu. 

Mtumishi mmoja alikuja na kunieleza jinsi ya kuwadanga waumini kwa kuwatabiria ili awakamue, nikaamwambia hilo kwangu haliwezekani kabisa. Mimi nataka nile taratibu na sitaki nile kwa mkupuo,. Mimi siwezi kumuibia mtu auze nyumba au afanye nini au mtu anishauri nifanye hivyo, nasema mtu huyo hatasimama na mimi madjhabahu moja. Nataka niwaambie ndugu zangu kuwa uchafu huo upo. Watu wanachukua mifano, wengine wanatembea na vidawa Fulani mikononi na utakuta wanakuwekea kichwani, na mara unaona damu zinatoka kichwani, huo ni wizi na uongo.

Unapoona mtu anahubiri usichukue tu mahubiri angalia na hali yake kama inafanana na acho hubiri. Watumishi wengine wana-“copy” mahubiri, na wengine wanachukua mahubiri ya akina Oyedepo kwasababu mahubiri yao ni “Wisdom” Anavyokuhubiria kuwa unakwenda kutajirika unaangalia na viatu vyake na anapokaa, Jamani hata macho huoni.

Ninawashauri wahubiri ukiona mambo yako hayajanyooka usihubiri mambo ya mafanikio, hubiri uaminifu ili watu wa-“Take serious”. Wanataka kuhubiri mafanikio tu wakati kuna mambo mengi ya kuhubiri. Msichukue meseji za watu na kuanza kuhubiri. Unaona mtu kanunua gari na wewe unasema, “Kwa mbinde zozote nitanunua gari”, nakuambia utapoteza muujiza wako. Mungu atakubariki kwa wakati wake. 
Ndio maana hata Isaka alimuuliza mwanae Yakobo, “Mbona umewahi umeleta mboga hii mapema?” Kwasababu alielewa uhitaji ni kazi ya kukesha. Lakini unaona mtu dakika kumi jambo alilotaka limekuja na ukimuuliza anasema, “Bwana ameniandalia”.

Watu wengi sana wanapata vitu kiulani na kuwadanganya watu kwasababu wanalegeza maandiko ya Mungu kupitia Biblia. Kwasababu Isaka alipokuwa akimshika Yakobo akasema, “Mwili huu ni wa Esau lakini sauti ya Yakobo”, alionyesha kushtuka. Halafu Yakobo akamchapa andiko, “Bwana ameniandalia na amenifanikisha”.

Ni lazima uwe muangalifu kwasababu kuna watu wanajificha kwa jina la Bwana, na ndio maana Mungu amekutaka wewe usikie sauti ya mchungaji. Hata kama mtu atasema nimeonyeshwa na Bwana na kuna mapigo yatatokea nyumbani kwako, toa sadaka hii usikubali kwani Mungu hawezi kuonyesha kwa Baba wa kambo wakati una baba mzazi.

Kila kanisani huwa na mpangilio wake, kila “jeans” lina mguu wake, sasa kwanini taarifa yako iende nyumba ya jirani na mama yako asijue, na wakati Mungu amempa nguvu ya kulivuta kundi? Basi unapopata meseji za watu wa namna hii ujue hizo meseji ni feki. Mungu hawezi kuleta meseji za kukuua wewe, ukiona hivyo ujue hiyo meseji feki. Kwasababu Mungu anafuata ile neema “inoder” jambo la aina yoyote lazima lifike, na likifika hata lingekuwa ni gumu kiasi gani, wazo la mchungaji atakalolitoa lazima limalize shida hiyo, kwasababu Mungu anamtumia mchungaji wako kama wakili wako wewe.

Sasa hizi nyota zinawafanya watu wengi waumie, lakini mimi nisema, “ Kuanzia sasa uangalie nyota ya asubuhi” Nabii yoyote akikuletea ujumbe wowote uwe wa kufa usipinge lakini uchukue na upeleke kwa mchungaji wako. Unajua watu wanakwenda na “seniority”. Kwamfano atakapotokea kijana yoyote akakutabiria kitu ovyo, na kikakuumiza moyo wako, na akataka ku-“comfirm” , na akatokea mchungaji wako akasema sio, basi amini sio. Mungu anaangalia “Senior between that person and your pastor”.

Kuna agano la Rehema ambalo linasemama juu yako, utakapo kuwa umefanya kosa kwa bahati mbaya, angano la rehema linakulinda. Utakapoingia katika misukosuko ya kukuletea hatari agano la rehema linakulinda. Mungu akakupe rehema ndani yako, ndoa yako, maisha yako, mipango yako. Kwa miezi hii sita Bwana akaangalie agano la rehema.

Katika amri za Mungu tunapenda ile amri ya kwanza naya pili. Mimi ndimi Mungu wako usiabudu miungu mingine, lakini kuna amri ya nane, tisa na kumi. Ninachotaka kusema ni kwamba Mungu atakupenda, atakukaribia na atakupongeza. 
Ninachotaka kukutia moyo ni kwamba lazima ufanye kazi na utajirikie ili ukifika mbinguni usemi kweli duniani lifaidika na mbinguni nafaidika, sio wewe uteseke duniani na mwisho wa siku mbinguni nako usikuone au ukuone. Ninachotaka kusema unaweza kuwa maskini duniani na mbingu ukafika kama alivyokuwa Lazaro.

Kuna watu wengine wanakonda sio kwababu ya kukosa chakula ila ni usongo wa maisha na stress. Utakuta mtu anapata taarifa kuwa nyumba ya mama yake imeanguka, mara watoto kodi, mara kuna mgonjwa, na yeye anaishi nyumba ya kupanga na kodi imekaribia. Ninakuombea kwa Mungu akakuondolee usongo wa mawazo kwa jina la Yesu. 
Kwasababu moyo ukishakuwa mzito, unakumbana na “depression” , lakini kuanzia leo Mungu akafungue moyo wako. Ninachotaka kukuambia kuwa kwa kupitia semina hii, utakwenda kufurajhia hapa duniani na utafurahia mbinguni. Bwana akakufanikishe ukawe mwepesi.

NYUMBA ZA KUPANGA.
Ninataka kutoa notice kwa wote wanaoishi nyumba za kupanga, kabla ya kufika mwakani uwe na nyumba yako. Wewe umekuwa mtu wa kukaa kwenye nyumba zako kama mlinzi. Mungu hakusema ulinde nyumba bali jenga nyumba. Unakulakula chocolate na unaendelea na mambo yako, umesahau kujenga nyumba.

Hakuna kiu ambacho umekifanya ambacho ni “touchable”  yaani kinagusika. Umeshika Neno, “Usisumbukie ya kesho” yatakushinda mwanangu. Kama wewe hutaki kujenga nyumba kwanini unakaa. Unakuta jamaa linawatoto kibao kwenye nyumba ya kupanga na ukimuuliza kwanini hujengi, anasema, “Sisi ni wapitaji”, sasa kwanini unazaa wakati wewe ni mpitaji? Ninaona hapa ninakuudhi.  Na wengine wanamlazimaisha hata mama asifanye kalenda. Hujasoma katika Biblia, inasema, “Asiyemtunza wa kwao ni sawasawa na asiyeamini” Ukimwambia basi hata katika nyumba jya kupanga weka vitu ndani ili nyumba ipendeze, mtu anaanza kububujika, na baada anakuambia, “Usiipende dunia na vyote vilivyopo”. Huyu mtu ana matatizo, kama hutaki kufanya hivyo hivyo basi rudi kijijini, kwani mjini hapa watu wana ma-“flat Screen”, mafriji yamekaa kila mahali, wana vyombo vya maana, nyumba zao zinaviyoyozi.  Wewe unasema maisha magumu wakati watu wanajenga, unasema uchumi ni mgumu wakati watu wannunua viwanja,  unasema mwaka huu hautuelewi wakati watu wananunua magari. Mungu akusaidie.

Kwenye nyumba ya kupanga hauwezi uka-“Control” mbu. Mbu utawathibiti kwenye nyumba yako mwenyewe , maana ukipuliza dawa unafunga kwasabu ndani kuna AC. Lazima utoke kwenye nyumba ya kupanga.  Leo watu wanaoishi kwenye nyumba ya kupanga tunawapa “Pressure” Ngona nikupe andiko,  Methali 24:3-5., “Nyumba hujengwa kwa hekima na kwa ufahamu huthibitika na kwa maarifa vyumba hujazwa vitu vya thamani na kupendeza” Sio unajenga nyumba unaweka kama “store” wakati ni chumba cha kulala. Unatakiwa ukienda “store” unakuta vyakula vimejaa, mchele umejaa, ukija “sitting room” unatamani ukae kwababu kunakuvuta, “coach” halikuumizi.

wewe Mungu amekupa nguvu, unashindwa hata kujenga, kuongeza duka la pili na la tatu, umeng’ang’ania mshahara wako wa manispaa, na hujui kama utatumbuliwa au vipi! Sasa adui yako mkubwa kuanzia sasa ni kutumbuliwa. Lakini jitu laenye hekima lina nguvu na lenye uwezo, lina njia nyingi za kuongeza mapato, ukilitumbua hapa linapata pale. Tatizo lako wewe huna nguvu na ushahidi upo, kwani sebule yako ovyooo, haijakaa kiblia, mgeni akija unaanza kuwaambia wanao, “Mzuieni kwanza” halafu unaanza kufunika makochi na mavitambaa. Ninakuuliza kwanini unafunika? Watu wenye nguvu hata uingie saa 12 asubuhi nyumba yao ndani imetulia, unaanza kujiuliza imepigwa deki saa ngapi?


Ninamuomba Mungu akakutie wivu leo, kwenye hilo eneo ukahame, jenga nyumba yako. Ninavyosema hivi, mwingine anasema, “Ushindwe”. Unatakiwa kujiangalia kuwa na uzee unakuja hivyo, wewe umebaki tu unaona raha. Wengine wamejiahau kwenye nyumba za serikali.

Usimsifu mwanaume kuwa ni wa maana sana kabla hujaona mke wake na watoto wake wana maana. Unapomsifu mtu angalia watoto wake, na uje huyu yuko kwenye “class” A, B au C. Wewe unaona raha tu wakati siku zinaenda wakati Mungu amesema lima, jenga. Mwaka wa 20 huu unasema nitajenga, na wanaume  ni watu wa ajabu sana, wakiulizwa na wake zao lini utajenga? Wanasema, “Ni siku moja tu shapuu nitakuwa nimemaliza” na miaka inakwenda. Mwanamke anamwambia tununue mfuko mmoja mmoja kwanza mume wangu, yeye anasema, “Acha nayo hiyo, nina mipango mizito kabisa, miezi mitatu nyumba imekwisha” Sasa unashangaa miaka inapotea.

Mwanamke unapoona hivyo ujue mumeo hana nguvu, hana uwezo. Ninajua nimekuudhi. Sikiliza nataka nikueleze, Biblia inasema, “Umpende Mungu wako kwa moyo wako wote, akili zako zote, nguvu zako zote”. Lakini sisi nguvu za Mungu tumezikunja na akili tumezikunja.

Na ndio maana kuna watu wengine wanataka hela za miujiza kutoka makanisani, ila wajanja wanaomba nguvu ya kufanya kazi. Hata huyo ndugu yako anayekusaidia kuna kipindi atachoka, ila amakuonea haya kukuambia, ila dalili ya kukuchoka utaona mchuzi siku ya kwanza unakuwa mzito na manyamanyama kwenye bakulia, lakini siku zinavyozidi kwenda unaona matembele mara jipikie mwenyewe, ukiona hivyo ujue ni dalili hizo za kuonyesha huyo bwana amechoka. Siku ya kwanza unaingia kwenye friji unachukua soda bila shida, ila siku zinapozidi utasikia jamani hizo soda ni za watoto sisi tunywe soda ya rangi, ukiona hivyo ujue amekuchoka unatakiwa kuondoka kwenye nyumba.


Wewe unaishi kwenye nyumba ya dada yako halafu unaimbaimba tu ukiwa bafuni eti, “Halleluya”, wewe nyamaza. Anayetakiwa kuimba akiwa bafuni ni mwenye nyumba (Provider). Wewe ukiwa bafuni na maji ya baridi unajimwagia unatakiwa kujikaza tu na sio kupigapiga miluzi. Anatakiwa kupiga miluzi ni “provider” anayenunua vitu ndani, hata akioga huku anaimba huku anacheka kwababu anangojea mgao. Wewe uko kwenye nyumba ya dadaako halafu unaimbaimba utasikia, “Kelele huko kaa kimia”. Na ukiona hivyo ujue amechoka. Sasa wengine wanaanza kusema, “Dada hanipendi” sio hakupendi ila amekuchoka. Huwezi kukaa kwenye nyumba ya mwenzako na bukta yako huku umevaa kavesti, utasikia mwenye eneo anakwambia, “Kavae shart”. Anayetakiwa kukaa kukaa kifua wazi ni mwenye nyumba.

Ninasema kunyanyaswa huko kukaishe kwanzia leo kwa jina la Yesu. Huu si wakati wa kunyanyaswa, ila anayekulealea amechoka
watu wengine ndefu zimeshuka hadi chini lakini bado wanalishwa tu. Ninaomba sana Mungu akakufanyie mambo makuuu, wasio na afya wakapokee afya zao, wasiokata tama wakapate kufanikiwa, uadilifu ukapate kuwa juu yako, ukapate kazi.

Kanuni moja ya Mungu inasema, “Asiyefanya kazi na asile”. Kama watu wa Mungu leo tutaishi Kibiblia au maagizo yanavyosema, hakuna mtu atakuwa maskini. 


Watu wote wanaoishi katika nyumba za kupanga hiyo ni “Special Notice”. Na maombi anayokuombea mchungaji wako ninaomba yakapate kutokea. Unatakiwa kuwa na harufu harufu na anayekuongoza.

Ukiona dada yako amekuchoka usimchukie kwani hiyo ni giza ya mafanikio yako. Ninakushauri hata kama umeishiwa namna gani usiuze nyumba ya urithi,  watu hawauzi mashamba wala nyumba ila wanatafuta mashamba na kuwekeza mashamba. Na ndio maana na mimi ninamuomba Mungu akuingize katika nyongeza, na wale ambao afya zao ni mbaya, neema ya Bwana ikakushukie ukafanye kazi, na ukishafanya kazi unanunue viwanja na baadae unajenga nyumba, na hilo ni agizo la Jehova. Na wabab muwe waangalifu sana kwasababu huwa wanasema, “Nitafanya One day” na miaka inaenda na watoto wanazeeka. Lakini akina mama huwa wanaenda mwendo mdogo mdogo na maombo yanakwenda na kueleweka. Nataka uwe mzizi. Na kitu kiubwa zaidi utakapokuwa mwaminifu, ukafanya kazi, ukawa na kiu ya kujenga nyumba, na ukawa mwaminifu kwenye mafungu yako ya kumi, ninajua lazima utafanikiwa.