RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DASTAN MABOYA ACHUKIA WATU WANAOKAA VIJIWENI BILA KAZI NA KUWA WATEGEMEZI, KATIKA SEMINA YA MID-CROSSOVER AFUNDISHA JINSI YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI


Bishop Danstan Maboya siku ya Jumatano 29.06.2016 katika semina ya Crossover Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema, ”Bwana Yesu asifiwe, nilitaka nikukumbushe kuhusu huu mwaka 2016 tutaendaje.
Bishop Danstan Maboya

Naomba tusome Kumbukumbu la Torati 11:10 Kwakua Nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, ulivyokua ukipanda mbegu zako humo na kuinywesheleza kwa mguu wako, kama shamba la mboga; Lakini Nchi ya vilima na mabonde, nayo hunyweshwa maji ya mvua ya mbinguni ; Nayo ni nchi itunzwayo na Bwana , Mungu wako; macho ya Bwana Mungu wako ya juu yako tangu mwanzo wa mwaka hata mwisho wa mwaka yaani kuanzia January mpaka December 2016.
Tunamshukuru Mungu kwa vitu vingi ambavyo ulikuwa huvitarajii, na wakati ulipokuwa unakuja kwenye mkesha wa Mwaka mpya nafikili kuna malengo uliyaweka, alafu kwa bahati mbaya yakachelewa kwasababu hakuna jambo lolote utakalo muuliza Mungu asikujibu baadaye akasema ya kwamba nitakupa haja ya moyo wako. 
Sasa nataka nizungumze katika yale matarajio ambayo mwingine ulikuwa huyategemei kwenye mwezi Machi, April, Juni hayajatimia basi katika Mungu yanakwenda kutimia kwasababu Mungu wetu anaangalia kuanzia Januari mpaka Decemba anasema nchi yapendezwa na milima na mabonde inamaana kwake ni kulima tu, anataka kukupa milima na mabonde, na mabondeni ndio tunalima mpunga tunalima vitu vya kila aina kwa lugha nyingine Mungu katupa nchi ya kilimo lakini ni kipi cha faraja?

Tunachomuomba Mungu ni kuona Mungu yupo pamoja nasi kuanzia January mpaka Desemba na ninajua yakwamba lolote ulilokuwa unalitegemea ambalo limekuja kwa uchache au halikuja kwa ule msisitizo nataka kukwambia Jehova shama anakwenda kuinua kwa ajili yako na ndio maana anasema msizimike mioyo mtavuna mlichopanda. 
Biblia inasema kilichotwaliwa kikichelewa moyo una ugua ule utabiri kazi nzuri na kila kitu lakini kunajambo alikuwa analitarajia ambalo linakwenda na umri unakwenda nataka uwe na moyo wa shaba kila siku Mungu atatengeneza jambo na Yeye anasema, “Niamini mtaona wema wa Bwana katika kila jambo unaloniandalia mimi tu”. 
Usisikilize maneno ya watu wewe sikiliza sauti ya Jehova. Ninayo mifano mingi uzazi mgumu ulikuwa kwa Rebeca mtoto wake akazaliwa akawa Nabii. Watu wenye uzazi mgumu wana bahati ya kupata watoto wazuri na wenye akili sana. Kwa sababu hiyo mtoto wako anaenda kuwa kiongozi katika nchi hii kwa Jina la Yesu Kristo. 
Tatizo wewe unasikiliza habari za watu hutaki kumsikiliza Mungu. Mara mjinga anakuwa hana mwelekeo. Hivi ni vitu vya kuweza kuelewa Mungu akisema ndio ni ndio na neema yake itaweza kusimama kuanzia leo. Usiogope uganga wala uchawi kwani una neema yakutosha juu yako. Soma Mithari 14:15 Mjinga huamini kila neno, bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.

Wewe uliyebahatika kwenda hospital unatakiwa kumshukuru Mungu kwaajili ya ma- “doctor” kwani akili wanazofanyia kazi ni Mungu amewaweka si kwa kinyume na “medicine”. Mungu amewapa akili ma- “doctor” ili kutusaidia sisi tusio na imani za kupokea muujiza yaa moja kwa moja. Lakini unaweza kukutana na “doctor” alafu kichwani kwake kuna mdudu amemuingia anaweza kukwambia eti, “huna maisha marefu kuanzia sasa”. 
Doctor mara nyingi anakupa majibu ya ugonjwa wako kwa kutumia elimu yake na akiangalia umri wako umefika miaka 48, anaanza kusema, “naona kuzaa kutakua kugumu” Unatakiwa kujua kuwa wewe huondoki kwa mwendo wa madaktari bali unaondoka kwa mwendo wakina Sarah na Ibrahim ambao mpaka miaka 90 anapakata mtoto. 
Huwezi kuondoka miondoko ya kawaida, bali unatakiwa kuwa jinsi ulivyo. Ukitaka kusikiliza kila neno unalombewa utaona kama wanakuchanganya vile, na ukiona hivyo unaamua kuhama kanisa mara uko Morogoro na huko utakutana na mtu anaanza kukuambia neno na baadae unaona halijafanya kazi kwako, utaanza kusema ngoja niende sehemu fulani utasikia hiki na hiki. 
Nataka nikuambie kuwa yatakushinda mwanangu. Lakini wajanja wanamngoja Bwana na ndio maana unaweza kukutana na mtu anakupa “record” ya watu walio mhudumia ni karibu watu 30, utafikiri kama vile Mungu hayapo kumbe “issue” siyo Mungu “issue” ni wewe kutuliza muhangaiko unaohangaika nao. 
Unapohangaika kutafuta watumishi inaonesha wewe huna IMANI, na kama una imani basi inaonesha humuamini kiongozi wako na ndio sababu unanyumba. Ila ukiamini kuwa kiongozi wangu ameitwa na Jehova na ana nafasi kwenye maisha yangu nasema, lazima muujiza utendeke kwako. Hata ukiona biashara zako haziendi basi ujue hujafungwa na mtu wewe bali ni wewe mwenyewe huna bidii. Ni watu wenye bidii tu watashikamana.

Naomba tusome Mithari 21:5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu, bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji. Kuna watu ambao wao wanachowaza ni utajiri tu wanajua kutumia muda, wanajua kutulia halafu wanapenda kusikiliza ushauri na ndio maana siku zote huwa wanapenda kuchagua watu wa madhabahuni. 
Kondoo mara nyingi husikia sauti ya mchungaji kwa sababu mchungaji hawezi kukupa ushauri wa haraka haraka ”Shalow shalow” kwa maana anajua akikupa ushauri huo unaweza kubuma na ukibuma kwako na upo hapo kanisani kwa mwaka mzima, itafika kipindi utamuuliza mchungaji wako kuwa, “mbona issue imebuma?” utamkaba koo mbona mambo yangu hayaendi. 
Mchungaji mara nyingi hutulia mahali pamoja ila baadhi ya manabii na mitume huhamahama makanisa wakihubiri, kwahiyo mtu kama huyu kumkata unapoona mambo yako aliyokutabilia yamegoma au yamebuma inakuwa ngumu sana. Yale majibu ya haraka haraka utayapata mitaani, utakuta mtu anakwambia miezi miwili unatajirika lakini baada ya miezi miwili tena unaona hola hakuna jibu. 
 Siku moja nilikuwa Marekani, mwenyeji wangu akaweka matangazo kila sehem ili watu waweze kuhudhuria. Watu walitoka sehem mbalimbali, mama mmoja alikuja pale nusu nisiendelee kuhubiri katika ule mkutano. Yeye alipofika pale alianza kusema, “nyie wahubiri kutoka Afrika mnashida mno mna njaa sana halafu ni wezi na matapeli”, aliniudhi sana mbele za watu nikauliza, “kwa nini unakasilika na mimi ni malaika wa Bwana?” akasema, “wote ni wamoja mwangalie sura yake”, na hapo nilikuwa nimebakiza nusu saa tu kuanza mkutano. Nikamwambia, “nimekuja kwajili yako wewe” na hapo hakuna aliyejibu. Unapofanya jambo fanya kwa bidii na kujiamini na usikatishwe tamaa na watu. Jiamini na jione wa thamani kuliko mwenzako hata kama ni tajiri kukushinda.



Taji ya wenye haki ni mali zao yaani mimi naweza muuliza ndugu Komba hebu nioneshe taji lako ataniambia njoo kesho nitalileta. Onyesha taji lililopo, kuna mambo mengine mengi ambayo tunatakiwa kuyaangalia Taji ni la wenye hekima ni mali zao na ninamuomba Mungu kwa ajili yako nikiungana na mbeba maono Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwamba kwenye awamu hii ya pili ya kuelekea kumliza mwaka, Bwana atakupa ”suprise” Bwana akakuvishe taji na ukiwa na wale waliokusema, wale wa nje ndio watakusema ni mpango wa Mungu aweze kutufanikisha na aweze kutuinua. 
Nataka nizungumze na moyo wako kwa sababu kuna kitu Bwana anakwenda kutenda leo. Mithari14:10 moyo huujua uchungu wa nafsi yake wala mgeni haishiriki furaha yake. Moyo unaweza kuujua uchungu wa nafsi lakini jirani yako au mtu yoyote hawezi kuujua. Amini kinachoongelewa na mchungaji wako, mchungaji wako mara nyingi huja kanisani kila Jumapili akiwa amebeba meseji tatu ili mmoja ukiharibika njiani atoe nyingine lakini Mwinjilisti yeye hubeba ujumbe mmoja”. 
Ni kazi ngumu sana kuishi na mtu akakuelewa wewe akailewa familiya mwaka mzima kama mchungaji anavyoweza kuishi na kanisa lake, “is a miracle”. Ninaomba Mungu akakutie nguvu katika awamu hii pili ya miezi sita ijayo kumaliza mwaka. 
Bwana akakutajilishe, Bwana akafanye mema Bwana akafungue akili zako, Mungu akapate kukustawisha na Mungu akujaze hekima katika upande wa biashara, ninaomba Mungu akafungue katika njia tofauti kwa maana Mungu anataka upanue hela yako ujiweke vyema. 
Mithari3:13 Heri mtu Yule aonaye hekima ,na mtu Yule apataye ufahamu, maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha , na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi Mungu yupo mbele na anahusika na biashara yako na mpango wake aweze kukuinua katika yote uyafanyayo.

“Namuomba sana Mungu katika neema aliyoweka kwa watumishi wake ikapate kuingia kwenu, biashara yako Bwana anakwenda kuisimamisha, biashara yako Bwana anakwenda kuiinua. Mungu anaona jinsi unavyo hangaika, Yeye anaelewa jinsi unavyopata taabu, anaelewa watoto unalea peke yako. Bwana anasema anataka kuinua biashara yako na iweze kung’aa Mungu akakufungulie milango ya tofauti. Wale waliofanya biashara za magendo wanakwenda kuwa na maduka, wale waliokuwa na migahawa wanakwenda kuwa na hotel, wale waliokuwa wamechoka wanakwenda kuwa juu. Sema kushoto kwangu ni utajiri na heshima na nina wingi wa siku Bwana akupe nguvu ya ziada.