RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWAOMBA WATU WAMSAIDIE KUWAKAMATA MBWEHA WADOGO WADOGO WANAOHARIBU KANISA

Siku ya Jumanne 28.06.2016 ikiwa ni siku ya pili ya semina ya Mid-Crossover katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuhubiri ujumbe mzito wa kuwaonya watu kutowadanganya wenzao na kuwapotosha katika safari yao ya kwenda mbingu. Sasa naomba usome ujumbe huu mfupi kutoka kwa Bishop, alianza kwa kusema, Bwana Yesu asifiwe, nawapenda na ninalipenda kanisa, na nimekuwa nikijitoa kwaajili yenu, na inafika kipindi nakosa hata raha kwaajili ya kanisa hili, na muda mwingine nashindwa hata kupata usingizi mzuri nikifikiria kanisa. 
Mimi sijui kitanda changu, ninalala chini kwaajili yako. Mnakumbuka Yule kijana kichaa aliyerusha kitanda changu mitandaoni?. Ninakitanda kizuri lakini silali kwenye kitanda, nilala chini, ninalia ninaomba, usingizi wa ngu ni kama sungura, nikipata usingizi kidogo mara nimeamka nipo macho, ninaanza kuhangaika huku naangalia mahubiri ya mtu na ninatiwa moyo au ninasoma Neno la Mungu, na ninahangaika hivi kwaajili ya kanisa.



Mimi ni mtu wa masafa marefu, nilikuwa naenda Marekani mara nne au mara tano kwa mwaka lakini tangia nimeanzisha kanisa hili la Mlima wa Moto ni kama nimeolewa na kanisa, sina raha ya kwenda Ulaya nikafurahi. Siku zote lazima niwepo kanisani, nakosa hata usingizi, kila wakati macho kosokoso, kinachonizuia ni Mungu mwenyewe amenifunga na kuniambia lea kanisa langu, lisha kanisa langu na tunza kanisa langu.

Watu walikuwa wanasema huyu ni CID au shushu au ni mama usalama, kwasababu kila wakati yuko Ulaya. Na nilipokuwa mbunge Dodoma kila wakati nipo bungeni mara nipo kanisani kwenye mkesha, mara Jumapili nipo kwenye ibada. Jamani mimi ninalipwa nini? Na kama nilikuwa nalipwa, mimi nani kwako, Je, ni mama yako? Si Mungu tu amenipa mzigo kwaajili yako.


Halafu ninapohangaika na kanisa, utaona mtu mwingine anaingia na kuanza kuchukua watu niliowalea na wakatulia. Utakuta anasema, “Twende kule kuna Nabii” Anaanza kuchukua watu wa kanisani kwangu ambao mimi niliwahangaikia kuwalea kanisani. Unafikiri kuwaleta watu wakae kama hivi na wakatulia ni kazi ndogo, Je, si Roho wa Mungu amehuskia jamani? Sasa watu wengine wametulia utaona mtu mwingine na kihelehele (zambi zabina). Eti Mungu yuko huku, Je hapa Mlima wa Moto hapana Mungu?



Kuna watu wengine wanawaonea watu kwa kuwasumbua kutaka kukopa. Utakuta mtu anasema “ee mama Patricia naomba unikopeshe au naomba unisaidie” Watu wapo tayari kukopa kwaajili ya Bwana na sio kwamba wana kiasi kingi ila wanajitoa kwa Bwana. Jamani achene tabia hiyo mbaya. Kwanini watu wanakuwa na wivu na Mungu? Mtu amebarikiwa na yeye anatoa kwa Mungu ili Mungu wake azidi kumbariki, lakini wewe unachukia unapoona huyu mtu anatoa kwa Mungu. Kwanini unakuwa na wivu na Mungu

Watu wengine hawana hata haya, utaona wanawavizia watu wanajitoa kumtolea Mungu na kuanza kuomba wakopeshwe. Jamani mtu anajitoa kwa Bwana na sio kwamba ana pesa nyingi kiasi hicho bali amejinyima amtolee Mungu ili Mungu ambariki. Watu wengine wapo tayari kwenda hata benki kukopa ili wamtolee Bwana na ili wamfurahishe Mungu wao.



Jamani tumekaa kanisani kwa neema, na hapa tumechangamana ni kwa neema. Kuna watu wengine hatuwezi kuingia hata kwenye ofis zao. Unaingia ofisi zao unakuta masekretari wane wamejipanga, lakini ninyi kwa neema ya Mungu mnadharau watu mnaona ni watu wa kawaida.

Halafu mimi kama Askofu nimejitahidi kumsopusopu mtu, nimempa neno, nimemuombea, amesimama anisaidie kazi ya Bwana halafu unaona anamtoa kanisani kwa uongo wake. Nikamatieni mbweha hawa wadogo wadogo niwashughulikie wanaharibu kanisa, wanaharibu huduma. Utakuta mtu anakuja kwangu akilia kwa kukwazwa na watu. Ukiona mtu anakuja mwenye lengo la kukatisha tama huyu ni mbweha naomba nikamatie huyo wala usimfiche.

Wapo wasichana wazuri wazuri utakuta vijana wanashindwa kutongoza nje wanakuja kutongoza kanisani. Sisi kama wachungaji tumemhubiria dada wa watu, akaokoka na sasa anapendeza na duniani ameacha umalaya, sasa anakuja kanisani anakutana na Malaya wa kiume anasali anaanza kumtongoza, jamani huyu ni mbweha. Ninaomba mnikamatie mbweha wadogo wadogo.

Habari mbaya ni kwamba mbweha na mbwa wanafanana. Ukiona kijibwa na ukiona na baby mbweha utaweza kumuua mbwa kuliko mbweha kwasababu wanafanana. Mbweha wadogo wadogo wananfanana na watu wa kawaida tu. Unaweza kumuona mtu kama ni mtu wa kawaida kumbe ni mbweha kazi yake ni kuharibu mizabibu, anaangalia alisimama amuangushe, anaangalia anayejitoa amvunje moyo, anaangalia Yule anayeenda vizuri amuharibu, na mimi ninasema nikamatieni hawa mbweha wadogo wadogo nitawshughulikia.

Inauma sana, mimi mtu akianguka ninalia ila watu hawaelewi. Mimi ninakosa kula na ninakosa usingizi kwasababu ya mtu mmoja ambaye ameanguka, najiuliza kwanini haji kanisani?, ni nani amemkwaza? Saa zingine nampigia simu, “Uko wapi umekumbwa na nini?”. Leo nimefurahia kumuona Evans Liganga, sijui ulisafiri lakini hukuniaga. Unajua kwanini mchungaji wenu ninajua majina yenu? Kwababu mimi nitatoa hesabu ya maisha yako kwa Mungu. Mungu ataniuliza mimi, sasa nisipowajibika. Naomba umwambie mwenzako, Je, wewe ni mbweha mdogo mdogo?”



Watu wanapoona ndoa imesimama, wanatuma meseji mbaya ili mradi wafuruge ndoa. Watu wanatamani kuona watu wametengana, jamani mnataka kila mtu awe bachela hapa kanisani? Mnataka kanisa liwe la wasela? Si vyema wenye ndoa tuwatie moyo ili wawashike waume na wake zao?

Kanisa mar azote huwa hawakosekana mbweha wadogowadogo, na kama utawaona wakamateni muwalete kwangu au kwa wachungaji na watawashughulikia.


Wapo vijana wanatabia chafu ya kuwaumiza wasichana, utakuta wao wanajiona wazuri kuliko watu wengine, utaona anamchumbia huyu anamuacha, anakwenda na kwa mwingine anamuacha. Utakuta dada wengine ni wembamba sana ila watakapoolewa unakuta ananenepa, sasa utakuta dada wa watu alikuwa amejitunza kwa Bwana, na wewe ukamchumbia na baadae ukamuacha solemba, mimi ninasema hawa ni mbweha wadogowadogo, wakamateni vijana kama hawa, wanaleta umalaya kanisani. Kama una hamu ya wasichana nenda bar au pombe shop utakutana na wengi tu wanaosaka noti.





Ninaomba Mungu badilisha nia zetu katika mioyo yetu, Mungu uliyejuu naweka wote mikononi mwako. Ninaomba Mungu ukatende miujiza na ishara, katika jina la Yesu nimeomba..amen