MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE SIKU YA JUMAPILI 10.07.2016 ALILIA NA WATU WASIOFANYA KAZI NA SASA AMEAMUA KUANZISHA MFUKO WA MLIMA WA MOTO ILI WATU WAPATE MITAJI

Siku ya Jumapili 10.07.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kufundisha waamini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jinsi ya kujituma kufanya kazi na kuwa watu wajasiriamali na kuacha kurithika mahali ulipo sasa, alisema, “Mama wa nyumbani usilidhike, hakuna sifa ya mtu kuitwa mama wa nyumbani. 
Wewe umeolewa lakini umekuwa ni mama wa kubweteka tu nyumbani ukitegemea kupewa kutoka kwa mume wako. Mama wa nyumbani ana mikono na anaweza kufanya kazi, unaweza kuweka hata genge ukauza. Jitahidi kutafuta kazi kwa mikono yako na uache tabia ya uongo, umbeya na utapeli bali fanya kazi kwa mikono yako. Tengeneza pesa yako mwenyewe, jioni unapokutana na mume wako uwe na bamia na mume wako aje na mboga ya majani na sio vyote kumtegemea mume wako.
Biblia inasema katika Kumbukumbu la Torati 8:18, na hapo mtamkumbuka Bwana Mungu wenu kwani ndiye Yeye awapae nguvu ya kuwapatia utajiri. Kwahiyo utajiri sio kitu cha kulazimishia ila ni Mungu anakupa Nguvu ya kupata utajiri. Mungu anakupa mpenyo, njia, wazo, “idea” ya kufanya kitu ili uweze kuinuka au kutoka mahali ulipo. Hata sisi unavyotuona hatukuwa hivi bali ni Mungu aliyetusaidia.
Tuki-“Rewind” miaka 10 nyuma hatukuwa hivi, watu walikuwa wanajulikana kwa “shirt” nyekundu, utasikia mtu anauliza, “Hivi Yule kaka wa shirt nyekundu yuko wapi? Lakini leo Mungu ametuinua mpaka la leo tunabadilisha nguo kwa sababu tunaye Mungu atupaye nguvu ya kupata utajiri.

KWANINI HUNA PESA?
Unatakiwa kujiuliza kwanini huna pesa?, wakati Hagai 2:6-9 inasema, “Fedha na dhahabu ni mali ya Baba yako”, sasa kwanini huna? Na kwanini unakubali kukosa pesa?, kwanini unakubali kutokuwa na fedha?, Kwanini unawakasirikia wenye pesa?. 
Kuna watu wengine wakimuona mtu mwenye pesa amependeza, basi akipita mbele yake utaona anamwangalia kutoka chini hadi juu. Na mimi ninasema, “Utaangalia sana, na utabaki na wivu wako”. Ninasema, “ Utaendelea kusona namba, mwenye jeuri utakula jeuri yako”.
Kama wewe ni mtoto wa Mungu kwanini vya rohoni unataka kurithi na vya mwilini hutaki kurithi?. Na huwezi kurithi vya mwilini kama hufanyi kazi, ni lazima ufanye kazi na Mungu atakubariki. Mama mmoja alikuwa ananambia kuwa, “Acheni Mungu aitwe Mungu, kwani sisi tulikuwa tunauza mchele, na tukileta sokoni magunia yote yenye mchele yanauzwa na wenzetu inabaki, na wengine wanasema sisi ni wachawi”, na alivyosema hivyo nikamwambia, “Bwana anasema, 
Mimi nitabariki kazi ya mikono yako nab ado Mungu atakubariki hata ukileta magunia 40 utauza yote
Ukuu wa Mungu utauona ukiwa katikati ya watu wengi, na unapoona Mungu anakuinua kuliko wengine ndipo utasema, “Hakika Mungu yupo upande wangu”. Watu wengine hawamjaribu Mungu kwasababu ni watu wa manung’uniko, watu wa masikitiko, wamekaa wameshika tama, kila mtu anamachozi yake. Hata wanaume wanaojikaza kisabuni na tai shingoni. Siku hizi hata wanaume wanalia kwasababu hali ni ngumu.
MFUKO WA MLIMA WA MOTO 
Kama kanisa tumeamua kuanzisha MFUKO WA MLIMA WA MOTO, tunataka watu wakope pesa wakafanye kazi. Baba mmoja na ghorofa lake, walikuja wathamini wakathamini ghorofa lake lililoko bahari kuwa lina thamani ya bilioni 1.2, lakini huo baba akaja kwangu akanambia, “ Mama Rwakatare ninataka nikuuzie, unaweza kulipa polepole hata ikiwa miaka saba kwasababu ninalihurumia ghorofa langu kutokana na watu wa benki ambao wananindai milioni 170, na mimi ninaona heri nilipe milioni 170 kuliko liuzwe na benki”. Ninachotaka kukuambia hapa ni kwamba watu wanashida sana, unaweza kumuona mtu yuko kwenye mjumba mkubwa mzuri lakini anashida ya pesa, nap engine hana hata pesa ya kula.
Sasa ninachokuomba ni kufanya kazi, na usipofanya kazi unakwenda na maji. Mnaosoma nyakati, soma alama za nyakati, watu wanakula mlo mmoja kwa siku, wakila saa tisa wakati watoto wamerudi kutoka shuleni basi watakula tena kesho yake saa tisa. Kwahiyo ni lazima tushughulike na tusikubali kufa. Mungu alisema, “Hutakufa bali utaishi, usimulie matenfdo makuu ya Mungu”. Lazima uhakikishe unafanya kazi, na tumeamua hapa kanisani, kuwa tutakuwa na “Semina za Kwenda Mbinguni” na pia tutakuwa na “Semina za Kwenda Mbinguni” ili watu wainuke kiuchumi.
Kuna watu wengine wanakikazi kidogo wanafanya kama vile cherehani, na yeye ameridhika, na ukimwambia kuna mkutano wa Wajasiriamali utakuta yeye haji. Watu hawajui kuwa Roho huambukiza, njoo ukutanme na wenzako waliofanikiwa, na ukifanya hivyo Roho itaingia ndani mwako na utakuwa mjasiriamali mkubwa. 
Usiridhike na kibiashara kidogo ulichonacho halafu unajiita na wewe mjasiriamali, “Wewe mjasiriamali gani huna hata ndege!”, Mjasiriamali gani hata baiskeli huna, umebaki na hela ya kula tu na kula kwenye unabangaiza. 
Sasa unaposikia semina wewe njoo ujifunze. Ukisikia kanisani kuna watu wanapeana mikopo, wewe njoo, sasa si bora kuja kanisani upate mkopo kuliko kukopa benki na baadae ukashindwa kulipa na wakaanza kukuuzia ghorofa lako au mali zako. Ninachotaka kukuambia ni wewe kuamka. 
Tusome Nahumu 2:9, inasema, “Chukue Nyara za Fedda, za dhahabu, ni akiba isiyoisha na imewekwa kwaajili ya watoto wa Mungu. Bwana ametuwekea fedha ili tuweze kufanikiwa, ni sisi kuwa kwenye zamu zetu. Ukiwa na kazi hata kama ni ndogo namna gani, Mungu atapenyeza Baraka zako hapo hapo, na Mungu atakubariki. Fanya kazi leo, tafuta biashara ndogo leo, tafuta biashara ya kati leo na kama unauwezo tafuta biashara kubwa leo na USIOGOPE kwani mtaji unatoka kwa Mungu.
Sisi Mlima wa Moto Mikocheni “B” tumebahatika kuwa na ma-”Bankers” wengi tunaosali nao hapa kanisani na wamekuwa wakiwafundisha watu wengine kuinuka kiuchumi, kwa mfano mama Kasembe, Johanita Mramba, Gilberto, na wengine wengi, wanauwezo mkubwa sana wa kutufundisha. Unatakiwa kuwapa nafasi. Tunataka kuwa na semina ya akina mama, “AKINA MAMA TUAMKE!” angalau kila mama awe na gari yake, akina baba wawe na BIASHARA KUBWA.
Mungu amenipa mzigo wa kuwainua watu kiuchumi kuanzia Julai 2016 mpaka Desemba 2016 lazima kila mtu ainuke, apate hatua ya KIUCHUMI na sio kurithika mahali ulipo. Usirithike na hali ulioyo nayo, mimi ninataka uende juu zaidi kiuchumi. Ninataka kukuona umeshika pesa, na sio wakati wa sadaka unaenda chooni ukiogopa kuonekana hujanyanyuka wakati wenzako wamenyanyuka kwenda kutoa sadaka. Ni lazima tufanye kazi kwasababu ni amri ya Mungu. Biblia inasema, “Asiyefanya kazi asile”. Mungu asema, “Ataibariki kazi ya mikono yangu” ukisoma Torati 28:1-14
Mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Mzee Malya akisistiza watu kufanya kazi

Mch. Mama MgetaMch. francis Machichi

Mch. Elizabeth Lucas


Mwandishi na Picha: Rumafrica | www.rumaafrica.blogspot.com