RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BOKO HARAM 6 WAKAMATWA NDANI YA KANISA


Lagos, Nigeria

WATU sita kati ya 100 wanaoaminika kuwa ni memba wa kundi la kigaidi la Boko Haram waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Ulinzi la Nigeria wamekamatwa wakiwa wamejificha kanisanihuko Festac Jijini Lagos.

Zoezi hilo lilifanikiwa jana kutokana na ushirikiano wa raia wema wa maeneo ya karibu kutoa taarifa kwa jeshi hilo kuhusu kuwepo kwa watu waliyowatilia shaka wakiingia kwenye kanisa hilo lililopo mjini Festac kwa lengo la kujificha ilihali muonekanao wao sio wa kusali.

Washukiwa hao waliripotiwa kutafutwa na jeshi hilo tangu wiki iliyopita baada ya kufanya shambulizi na kutokomea huko mjini Maiduguri Borno.

Watuhumiwa waliokamatwa jana wametamnbulika kwa majina ya Ali Ibrahim, Ahmed Abubakar, Kamsalem Goigoi, Adams Ibrahim, Mohammed Ibrahim na Ali Blam Babagana waliokuwa wakitoroka kutoka Borno walikotekeleza shambulio.