RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CONFIRMED: FC BARCELONA IMEMSAJILI STAA MPYA NOU CAMP



Klabu ya FC Barcelona ya Hispania leo July 12 2016 imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine atakayejiunga na klabu yao kuanzia msimu wa 2016/2017, Barcelonakupitia tovuti yao wametangaza kumsajili Samuel Umtiti kutoka klabu ya Olympique Lyonnais.

FC Barcelona imemsajili Samuel Umtiti kwa mkataba wa miaka mitano, kwa dau la uhamisho wa euro milioni 20, Umtiti atajiunga na kikosi cha Luis Enrique na atakuwa akicheza nafasi ya beki wa kushoto au beki wa kati.

Umtiti ambaye katika mechi nyingine za Olympique Lyonnais alikuwa akicheza kama nahodha, amecheza jumla ya mechi 170 akiwa na klabu hiyo katika kipindi cha miaka mitano na amefunga jumla ya magoli matano, Umtiti ana umri wa miaka 22, mkataba wake na Barcelona utamuweka klabuni hapo hadi 2021.