RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DADA APONA UKIMWI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA PETER HOSPITALI ZAIDI YA MBILI ZA THIBITISHA HANA UKIMWI

Siku ya Jumapili dada mmoja aliweza kufika katika Kanisa la Yesu Kristo Huduma ya Maombezi na Uponyaji kwa Nabii Flora siku ya Jumapili 03.07.2016 kushuhudia jinsi Mungu alivyomponya UKIMWI, alisema, "Bwana Yesu asifiwe. Mimi niliathirika na ugonjwa wa UKIMWI. Na nilienda kupima mwezi wa 12 nikaambiwa nimepata virusi vya UKIMWI, nilipewa cheti cha kuhudhuria “clinic” na tarehe 20.07.2016 niliambiwa niende kuchukua dawa na imeandikwa kila baada ya mwezi niwe naenda kuchukua dawa
kulia ni dada aliyepona UKIMWI akiwa na Mch. July wa kanisa la Nabii Flora

Nimezunguka kwa Manabii wengi kama Kigamboni, Mbezi, Iringa kutafuta uponyaji lakini sikupata, nilikata tamaa,. Sasa siku moja nikawa nimechukua simu yangu na nikaingia google na nikaandika kupona UKIMWI, baada ya hapo nikaona imekuja picha ya Nabii Flora . Baada ya hapo nikamwambia mama kwasababu wazazi wangu ni Waislamu, nikamwambia mama yangu kwasababu baba yangu alikuwa hajui chochote,. Mama anakanambia nitakupa nauli uwe unaenda kwenye maombi, nikamkubalia.. Nakumbuka nilikuja kanisa kwa Nabii Flora mwezi wa Aprili 2016, nikakutana na Nabii akanambia Jumatatu uje tutaongea vizuri, na nilipokuja Jumatatu akanambia ninkupa siku 21, na mimi nikawa nahudhuria maombi kwa siku hizo zote 21 nikifanya maombi. Siku zingine naamka asubuhi natumia Joel 5:21, Zab 103 huku ninakunywa maji ya upako yalioombewa na Nabii Flora. Pia nilikuwa na jinni mahaba lilikuwa linanisumbua sana, basi nikachukua sticker nikaweka mfukoni, na kuanzia hapo lile jinni likapotea. Nilipomwambia mama kuhusu nauli akanambia mimi sina, nikamwabia naomba unitafutie nauli kwani mimi nataka nipone.
Nesi (kulia) aliyethibitisha kuwa dada aliyekuwa na UKIMWI KUWA HANA UKIMWI

Mwezi wa sita nikaenda “clinic” kuchukua dawa na nilipochukua nikamwonyesha Nabii Flora nay eye akaomba alishike kopo la dawa na akasema, “Hizi dawa ni mara ya mwisho kuzitumia” Basi siku ya Jumamosi nikanywa hivyo vidonge 20 kikabaki kidonge kimoja cha kunywa Jumapili. Nilipofika hapa kanisani kwa Nabii Flora siku ya Jumapili nikamuomba sana Mungu na zile sadaka anazosema nabii Flora tuzitoe nikawa nazitoa, na kila kitu akisema nifanye na mimi ninafanya hivyo hivyo.

Nabii Flora Peter akasema, “Ninaona watu 35 wamepona UKIMWI” na mimi nikatoka mbele.

Kuna nesi ambaye alikuwa ananipima ambaye na yeye ana mwanae anaumwa vidonda (nimekuja naye hapa kanisani) akaenda kunipima katika hospitali yao inayoitwa HARAFA iliyopo Kitunda jijini Dar es Salaam na akanikuta sina UKIMWI nipo “Negative”. Baada ya hapo nikatoka hapo hospitalini nikaenda AMREF, na nilipofika pale nikakutana na mtu aliyewahi kunipima akiwa kwenye mapokezi, nikampita kama smuoni. Nikaingia kwenye chumba cha kupima UKIMWI na nilipoingia humo nikapimwa na kuambiwa niko “Negative” Baada ya hapo nikamuomba Yule daktari aliyenipima na kuniambia niko “Positive” nikamwambia “siulisema niko “Negative”?, Lakini sasa nipo “Negative”, wakaanza kuchanganyikiwa na kuniambia niandikiwe barua nikapime kwingine. Baada ya hapo nikaamua kwenda hospitali ya Dar Group kupima tena, nilivyopimwa nikaambiwa “Negative”. Nikamuelezea historia yangu daktari, wakachanganyikiwa na kuanza kuomba namba ya Nabii Flora.

Baada ya nesi ambaye naye mwanae anasumbuliwa na vidonda akaomba nimlete kwa Nabii Flora