MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

DROGBA, PIRLO KUWAVAA ARSENAL MAREKANI

WACHEZAJI waliowahi kuwika na timu mbalimbali kwenye ligi kubwa duniani watashuka dimbani kupambana na timu ya soka ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza katika pambano litakalopigwa Julai 29 mwaka huu.

Mechi hiyo itapigwa kwenye uwanja wa Avaya uliopo San Jose, California. Kikosi cha mastaa hao kitakuwa chini ya kocha mkuu Dominic Kinnear na mechi itarushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha Sky Sports.
Didier Drogba.

Kikosi kamili kitakuwa ni kama ifuatavyo:

Makipa: David Bingham (San Jose Earthquakes), Andre Blake (Philadelphia Union)

Mabeki: Matt Besler (Sporting Kansas City), Steve Birnbaum (D.C. United), Laurent Ciman (Montreal Impact), Andrew Farrell (New England Revolution), Liam Ridgewell (Portland Timbers), Keegan Rosenberry (Philadelphia Union), Brandon Vincent (Chicago Fire), Kendall Watson (Vancouver Whitecaps FC)

Viungo: Kyle Beckerman (Real Salt Lake), Mauro Diaz (FC Dallas), Giovani dos Santos (LA Galaxy), Jermaine Jones (Colorado Rapids), Kaka (Orlando City SC), Sacha Kljestan (New York Red Bulls), Darlington Nagbe (Portland Timbers), Andrea Pirlo (New York City FC), Will Trapp (Columbus Crew SC)

Washambuliaji: Clint Dempsey (Seattle Sounders FC), Didier Drogba (Montreal Impact), Sebastian Giovinco (Toronto FC), Cyle Larin (Orlando City SC), Ignacio Piatti (Montreal Impact), David Villa (New York City FC), Chris Wondolowski (San Jose Earthquakes).