MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

HOFU KUKAMATWA KWA GWAJIMA, WAUMINI WASHANGAA
Askofu Gwajima.

KIONGOZI mmoja wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye hakutaja jina lake kwa madai ya kuwa siyo msemaji, amesema kuwa tetesi zinazotawala mitandaoni za kukamatwa kwa kiongozi wao, Askofu Josephat Gwajima hawana taarifa yoyote.

“Kama unavyoona hapa tunaendelea na ibada kama kawaida, hizo taarifa hapa hatuna, inashangaza” alisema.


Mtandao huu ulifika katika kanisa hilo eneo la Ubungo Maji, Dar kutaka kupata ukweli juu ya taarifa kwamba Askofu Gwajima amekamatwa na polisi.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kama wangekuwa na taarifa hizo wasingeendeleza ibada hiyo na maombezi bali wangekutana ili kutafakari hatma ya kiongozi wao.

Askofu Gwajima anadaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi leo mchana katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili akitokea nje ya nchi.

Tovuti hii yaGlobal Publishers ilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kutaka kupata ukweli wa taarifa hizo lakini simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Taarifa zaidi kuhusiana na tukio hili zitaendelea kuwajia kadri zitakavyokuwa zikitufikia.