MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

KAKA KUTOKA MWANZA AOKOLEWA KATIKA MAUTI BAADA YA KUOMBEWA NA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KWA NJIA YA SIMU

Siku ya Jumapili 17.07.2016  Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni katika ibada ya Kufunguliwa Kwako alikuwa na haya ya kusema na kushuhudia, alisema, "Bwana Yesu asifiwe. Ni watu wangapi wangependa miujiza itembee katika maisha yao? Miujiza ni chakula cha Mungu, kwahiyo kupata miujiza ni haki yako. Leo asubuhi nimepata simu ya ajabu sana kutoka Mwanza, mtu akanipigia akasema, “Mchungaji Bwana Yesu asifiwe”, nikamjibu “Amen” nakasema, “Mimi nimeponywa kwenye maombi yako ya simu uliyoniombea wakati naumwa sana, kwani nilikuwa nimelala nikitegemea kifo kunichukua wakati wowote, kwani watu wote walikuwa wamekata tamaa wakijua nimekufa. Mimi nilikuwa naona ndugu na marafiki waliokuwa wakiniuguza na kunitembelea wakisemezana juu yangu lakini nilikuwa sina nguvu ya kuwajibu. Nilikuwa nataka kuwambia kuwa, “No, I’m still alive” ila nguvu za kuwaambia nikawa sina”. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
Basi dada yangu akawaambia ndugu zangu kuwa ngoja tumpigie simu mchungaji mama Rwakatare Dar es Salaam, na walipopiga waliweza kunipata, “ akanambia, “Mchungaji hapa nipo Mwanza na kaka yangu yuko hoi na saa yoyote tunaweza kutangaziwa habari mbaya juu yake kwahiyo naomba maombi”. 
Alivyonambia hivyo, na mimi nikaamua kuomba naye. Sasa hivi tunavyoongea kaka yangu ni mzima wa afya njema, na ninakumbuka ulimuombea kwa simu ukisema, “Kwa jina la Yesu Kristo nakataa roho ya kifo, toka kwa jina la Yesu, mwaachilie kwa Jina la Yesu, aachilia uzima ushuke kutoka kwenye utosi hadi kwenye unyayo katika Jina la Yesu, pokea uzima, pokea afya njema” Sasa baada ya kuombewa, Yule kaka yangu akawa anataka ku-“smile” lakini hawezi, kumwambia kuwa, “Dada maombi ya mchungaji Rwakatare yamefika”. Lakini pale pale nilipoimaliza kuomba, akatokea daktari kuhakikisha kuwa ni mzima, akamwambia mgonjwa, “Kama ni mzima, ninavyoongea hivi fungua macho yako”, mgonjwa akafungua macho yake. 
Mgonjwa anasema alipofungua macho akawa bado hana nguvu, ila walipoondoa ndugu zake ndipo alipoanza kupata nguvu. Madaktari wakaja wakaanza kunitoa mipira na mirija niliyowekewa. Baadae akaanza kutembea kidogokidogo, na aliweza kufika hata chooni peke yake. Baada ya siku tatu akaruhusiwa hospitalini na kwenda nyumbani.


Kama wachungaji na kama wanadamu mara zingine tunachoka kuombea watu, unashangaa unapata simu mfululizo 20 lakini tunavumilia kuwaombea. Na hivi sasa ninataka tuwe wengi tunaweza kupokea simu za watu na kuwaombea, kwani kama kuna watu wanaweza kufufuka kwa kupitia maombezi yetu, kwanini sasa tuache kuwaombea eti tunachoka. Watu waliokata tama, katika kwa maombi wanaweza kuinuka tena. Kwahiyo usikate tamaa na usimkatie tamaa mtu. Mungu bado anampenda, Mungu bado ana haja naye.