MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MASTAA 100 WALIOINGIZA PESA WATAJWA, MAYWEATHER SIO NAMBA 1 TENA.. RONALDO, MESSI, KEVIN HART WAMETISHA
Orodha yenye utafiti wa mastaa gani wa dunia wameingiza pesa nyingi kwa mwaka mmoja uliopita imetoka na imechapishwa na jarida maarufu la FORBES ambalo limekua likifanya hivyo mara kwa mara.

List yenyewe yenye mastaa 100 walioingiza pesa ndefu inaonyesha nafasi ya namba 1 iliyoshikwa na bondia Floyd Mayweather mwaka jana imechukuliwa na mwimbaji wa muziki wa country Taylor Swift ambae kuanzia June 2015 mpaka June 2016.

Taylor Swift

Orodha hii inajumuisha mastaa wa kiume na wa kike kutoka kwenye area mbalimbali ikiwemo soka, comedy, uigizaji na muziki ambapo mastaa wengine tisa kwenye Top 10ni One Direction kwenye namba 2 wakiwa na $110 million, James Patterson namba 3 na $93 million Dr. Phil McGraw namba 4 na $88 million.

Kevin Hart


Staa wa soka wa Portugal na Real Madrid Cristiano Ronaldo yuko kwenye nafasi ya 5kwa kuingiza dola milioni 88, mwigizaji na mchekeshaji Kevin Hart kachukua namba 6kwa $87.5 million, namba 7 ni “king of media” Howard Stern na $85 million.

Ronaldo


Namba 8 imechukuliwa na staa wa soka wa Argentina Lionel Messi kwa kujipigia zake $81.5 million na namba 9 ni mwimbaji Adele ( $80.5 million) huku mtangazaji wa Radio Rush Limbaugh akishika namba 10 kwa USD 79 million.

Messi

Mrembo ambaye ni mke wa rapper Kanye West, Kim Kardashian ambaye ndio ametokea kwenye cover la toleo la jarida hili ameshika namba 42 kwa milioni zake 52 USD ambapo pesa yake kwa kiwango kikubwa mwaka huu imetoka kwenye mobile gameyake.

Jay Z na Beyonce

Wapenzi walioingiza pesa nyingi zaidi ni Beyonce (54 USD million) na Jay Z(million 53.5) ambapo kwa pamoja wamepiga USD milioni 107 huku kwenye 100 bora Jay Z ameshika namba 36 na Beyonce namba 34, Rihanna namba 13 kwa kuingiza dola za kimarekani milioni 75.

RiRi

Mkali wa basketball LeBron James amechukua namba 11 kwa kuingiza dola za kimarekani milioni 77 kwa kipindi chote hicho cha June 2015 mpaka June 2016.