MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCH. OTIENO. HAJIALISHI WAMEKUSEMA KIASI GANI LAKINI MUNGU ANAKUKUMBUKA SONGA MBELE

Mch. Otieno wa kanisa la Mlima wa Moto Bunju siku ya Jumanne 19.07.2016 katika semina ya Wiki ya Kukumbukwa na Mungu inayoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam Tanzania mpaka 24.07.2016 alikuwa na haya ya kusema, "Bwana yesu asifiwe. Jamani hii ni wiki ya kukumbukwa na Bwana. Haijalishi ni watu wangapi wamekushusha katika mipango yako. Wanadamu wanaweza kuongea juu yako, wanaweza wakakushusha, lakini siku ya leo ya kukumbukwa na Mungu, Bwana atakutoa chini na atakuweka juu. Bwana atakuunganisha na watu wanaostahili. Wewe waache wakushushe lakini waambie Bwana amekukumbuka siku ya leo. Na hii wiki utakumbukwa na watu waliokusahau watasema, “Kumbe yupo Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni"B"

 Mch. Otieno
 

 


 


 Mwandishi na Picha: Rumafrica