MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MLOKE AJIANDALIA KABURI MAPEMOLA
Mlokole akihojiwa nyumbani kwake.


Na Mwandishi Wetu, UWAZI

MWANZA: Mlokole aliyejulikana kwa jina moja la Mganga ameonesha maajabu kufuatia kuamua kuandaa sehemu ambayo atazikwa atakapofariki dunia, Uwazi linachimba zaidi.

Baadhi ya watu waliozungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, walisema kuwa, kitendo cha Mganga kujiandalia sehemu ya kuzikwa kwenye Makaburi ya Kirumba, kimewashangaza, hasa kwa namna alivyoliandaa kaburi lake.“Pale makaburini, amejenga kuta mbili zenye alama ya L. Kila ukuta ameandika maandishi ambayo anaamini ni ujumbe wake kwa wanadamu wote, lakini akionesha msimamo wake kuhusu imani yake ya kilokole,” alisema shuhuda mmoja.

Maandishi yanayosomeka kwenye kuta hizo ni; Yesu ndiye ltd (limited) wa kifo, kumbuka kutubu kabla ya kifo. Msipokuwa makini kila mwanaume atapungukiwa nguvu za kiume na kutofaa mbele ya mkewe. Kwa dhambi zenu vifo na njaa vitawala…


Mtoto wake aliyemwachisha masomo

Hata hivyo, Uwazi lilipomtafuta Mganga kwenye sehemu anayofanyia kazi, akiwa ni fundi wa kushona nguo, baadhi ya majirani walisema kuwa alikamatwa na polisi kwa madai ya kumkatisha masomo mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 8 kwa lengo la kumfundisha maandiko ya Biblia zaidi.

Uwazi lilifika kwenye Kituo cha Polisi Kitangiri alikokuwa akishikiliwa ambapo afande mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema: “Ni kweli Mganga amekamatwa. Anatakiwa kupewa ushauri wa kisaikolojia. Inaonekana kama hayupo sawa. Lakini mbaya zaidi, ni kitendo cha kumzuia mtoto wake kusoma.
“Mwaka 2015, alimwachisha shule mtoto wake, miezi miwili tu baada ya kuanza masomo, akamwingiza kwenye kusoma Biblia. Ni kweli, anaijua sana, lakini hasomi elimu ya kawaida jambo ambalo ni kosa.
“Mkitaka uhakika zaidi, mtafuteni dada wa Kipindi cha Nitetee Foundation, Flora Lauwo, anajua kila kitu kuhusu Mganga, mtoto wake na aliko mkewe. Maana nasikia alimfukuza mke wake akidai ni mzinzi.”

Uwazi, juzi lilimsaka Flora ambaye alikiri kukutana na Mganga na kuzungumza naye mambo mengi.
Alisema: “Mganga nimeongea naye, kwa kweli mambo mengi ni ya kushangaza. Sisi wanadamu bwana! Mtoto wake anajua kuisoma Biblia kuliko kawaida. Lakini amekuwa akimfungia ndani tu, hatakiwi kutoka.

“Akitaka kujisaidia haja ndogo, anatumia tundu dogo alilomwandalia. Hataki mtoto aende kwa mama yake, anaishi naye mwenyewe. Ilibidi mimi niite polisi amweke ndani kumchunguza.

“Kuhusu hilo la kaburi ni kweli kabisa, amejiandalia eneo litakapochimbwa na amezungushia kuta zenye maandishi. Mimi nitarusha mahojiano yake kwenye Kipindi cha Nitetee, Ijumaa hii kwenye Channel Ten.”