MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MSAJILI HAZINA ASEMA TWIGA BANCORP BADO IMARA


Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru, akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kwenye ofisi za benki hiyo zilizopo barabara ya Samora jijini Dar mapema leo.


Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa benki hiyo, Amina Lumuli (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Cosmas Kimario (kulia) wakiwa na Msajili wa Hazina.


Wanahabari wakiwa kazini.


Mkutano ukiendelea.

MSAJILI wa Hazina, Lawrence Mafuru, leo amewaondoa hofu wateja wa benki ya Twiga Bancorp hapa nchini kwa kutoa ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuhusu msimamo wa serikali kwa benki hiyo.

Msajili huyo alisema taarifa iliyotolewa awali na serikali ilieleweka vibaya kuhusu msimamo wa serikali kwa benki hiyo.

Alisema hivi sasa serikali inasubiri mapendekezo ya kitaalamu yatakayowezesha kutatua changamoto za benki hiyo inayohitaji nyongeza ya mtaji kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya kisheria.

Aliwaondoa shaka wateja wa benki hiyo na kuwaambia benki haiko katika hali mbaya ya kiuchumi bali ni nzuri na hata kama kwa bahati mbaya lolote likitokea, haki zao haziwezi kupotea kwani benki zote hapa nchini zinadhaminiwa na Benki Kuu (BoT). Hivyo aliwataka wateja waendelee kuiunga mkono benki hiyo.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL