MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MTANGAZAJI WA CAPITAL TV AUNGANA NA WAOKOVU WAPYA NA KUAMUA KUOKOKA SIKU YA JUMAPILI 10.07.2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwaajili ya hawa ndugu zetu walioamua kuokoka siku ya Jumapili 10.07.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kuongozwa sala ya toba na wachungaji wa kanisa hili. Baada ya kuongozwa sala ya toba waliweza kuombewa na baadae walipelekwa baharini kubatizwa. Mungu anazidi kuwalinda kwani siku ya Jumanne walinza rasmi masomo ya kukulia wokovu hapo hapo kanisani na baada ya hapo maombezi yatafanyika kuwalinda na maadui wasiwarudishe nyuma.

Katika safafri hii ya kwenda kwa Baba mbinguni, kulikuwepo pia na mtangazaji wa Capital TV ambaye naye aliamua kukokoka baada ya kuona rafiki zake aliokuwa nao mitaani wameokoka na pia kutokana na nafsi yake kumsukuma kuokoka.
Kushoto ni Mtangazaji wa capital TV akiwa na nguo ya kuvaa wakati wa kubatizwa

Sasa ni zamu yako wewe ambaye hujaokoka, kuokoka sasa. Mungu anakuita siku ya leo, umpokee awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Unaweza ukawa unapitia mapito magumu na usijue adui yako ni nani, lakini ukiokoka Mungu atakupa mwanga na utatambua mbaya wako na utaweza kumuangamiza. 


Mungu akubariki sana. Ibada zetu zinaanza saa 3 asubuhi hadi mchana hapa kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge Mataa, utaona gari letu la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

WAOKOVU WAPYA WAKIJIANDAA KUELEKEA BAHARINI KUBATIZWA


SAFAFRI YA KUELEKEA BAHARINI ILIANZA

 Hawa nyuma ni mtangazaji wa Capital TV na mke wake

WAKIFANYA MAOMBI KABLA YA KUANZA KUBATIZWA

WAKIELEKEA KWA WAINJILISTI TAYARI KUBATIZWA Mtangazaji wa Capital TV, wa tatu kutoka kushoto Mtangazaji wa Capita TV

Mwandishi na Mpiga Picha: Rumafrica