MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

PINDA KUZINDUA RASMI HELIKOPTA YA KANISA LA GWAJIMA WIKI IJAYO


Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kuizindua rasmi kwa matumizi helikopta mpya iliyonunuliwa na kanisa la Ufufuo na Uzima nchini chini ya mchungaji wake kiongozi Josephat Gwajima.

Tukio hilo la uzinduzi linatarajiwa kufanyika tarehe 9 November katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe jijini Dar es salaam ambako ndiko kanisa hilo lenye maelfu ya waumini linapofanyia huduma zake. Helikopta hiyo iliyogharimu mamilioni ya shilingi, inatarajiwa kutumiwa na kanisa hilo katika kazi za uinjilisti mikoani na vijijini, kazi ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kanisa la Ufufuo na Uzima ndilo linaloongoza kwa kuwa na waumini wengi ambao hufikia zaidi ya watu elfu 20,000 wanaohudhuria ibada kwa siku za jumapili nchini. Pia kanisa hilo pia ndilo linaloongoza kwa kumiliki vyombo vikubwa na vya kisasa kwa shughuli mbalimbali hususani mikutano, vyombo hivyo pia ndivyo vilitumika wakati wa mkutano wa muhubiri wa kimataifa Reinhard Bonnke ambaye aliwakilishwa na msaidizi wake katika huduma hiyo hivi karibuni.