RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RC MAKONDA AFAFANUA MPANGO WA KUIENDELEZA DAR


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amefafanua mpango wa mamlaka yake katika kuliendeleza Jiji la Dar es Salaam ili kuleta ufanisi, maendeleo na usalama kwa wakazi wake.

Makonda ameyasema hayo leo katika mahojiano na kituo cha radio cha Clouds FM cha jijini wakati wa kipindi kijulikanancho kama Power Breakfast.

Miongoni mwa mambo aliyoyalenga ni pamoja na kusisitiza watu kufanya kazi, kupiga vita uvutaji wa shisha, ushoga, na kuendeleza miundombinu mbalimbali kwa ajili ya huduma za wakazi wa jiji hilo.

Kuhusu usalama, kiongozi huyo alisema mamlaka ya mkoa yatafanya ukaguzi katika sehemu yoyote jijini kwa ajili ya kuhakikisha usalama na ulinzi wa wananchi, jambo ambalo alitaka lipewe ushirikiano na wakazi wote.

Akizungumzia ajira, alisema kuna mpango wa kuwachukua vijana zaidi ya 1,200 ambapo watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali ambao watapatikana kwa uchambuzi maalum.

“Tuna mkakati wa kuwachukua vijana zaidi ya 1,200 kwa ajili ya kuwapeleka katika mafunzo ya ujasiriamali, lakini ni lazima tuwatambue kwanza watu hao,” alisema.

Alidokeza kuwa kuna mpango wa kupanua muda wa kufanya biashara jijini tangu asubuhi hadi saa nne za usiku ili kuwapatia watu huduma kwa muda mrefu na kwamba kilichotakiwa ni kuimarishwa kwa usalama ikiwa ni pamoja na kuongeza taa sehemu mbalimbali za jiji.

Mambo mengine aliyozungumzia ni dhamira ya kuwawezesha walimu wa mkoani kwake waanze kusafiri bure katika mabasi ya mwendo kasi na kutowapa pesa ombaomba mitaani ili kuwafanya waondoke jijini.

Kuhusu maovu mbalimbali yanayofanyika jijini, Makonda alishutumu ushoga, utapeli na uvutaji wa madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na shisha.

“Ushoga umepingwa na vitabu vya dini na hakuna sheria inayoruhusu ushoga, kwa hili najua watu watanitukana sana lakini nguvu niliyo nayo hakuna wa kunisimamisha,” alisisitiza huku akiwaonya watu wanaojiingiza katika utapeli kwa kutumia majina ya watu wengine, likiwemo