MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

SOMO: CHAPA ZA KICHAWI - ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA

Neno chapa linatafasiriwa kama alama, mhuri au arabuni (Seal, Mark). Watu wengi wanashangaa ukiongea na kufundisha wachawi, majini, mapepo kwasababu Mungu hawezi kufanya kazi duniani bila kuwa na wakala wake ambaye ni Binadamu hata shetani hawezi kufanya jambo lolote bila kumtumia binadamu , mfano balozi wa Japan yupo hapa nchini lakini ni wakala anayewakilisha nchi ya Japan iliyopo mashariki ya mbali. Huwezi kumwona Mungu hata siku moja lakini ukimsikia Askofu anasema fahamu Mungu anasema kupitia yeye na hata wachawi nao hutumika kama wakala wa shetani kutimiza kazi zake lakini hawana kitu tena juu ya wanadamu.

Wahubiri wengi wamekuwa wakufundisha sababu za kutotoa sadaka au tabia mbaya au ujazo war oho mtakatifu au tabia za ulevi hizo zote zimetokana na shetani na wakala wake. Eliya alijitokea kwa mtumishi wa Mfalme aitwaye Obadia akamwambia mwambie Mfalme niko hapa mwambie aje, Eliya akamwambia ahabu ili kumaliza mgogoro waambie wanaomtumikia shetani waje na wale wanaomtumikia Mungu waje ili tuondoe kuondoa utata wa nani aabudiwe. Eliya mtishibi aliwaita manabii wa baali akawashinda kwa kushusha moto wa Mungu huku wao wakishindwa kushusha moto kwa mungu wao ili itofautishwe Mungu wa mbinguni ndiye anayestahili kuabudiwa.

Kuna makuhani ambao ni Binadamu wameamua kumtumikia shetani na kufanya mapenzi ya shetani hapa duniani kuharibu maisha ya watu na hao ukiwaacha wataharibu maisha ya watu kwa kuwawekea chapa za kichawi lakini ukiwapiga hao basi unaondoa matatizo yanayowakumba watu kwenye taifa. Ndiomaana ya kufundisha chapa za kichawi ambazo ukiziondoa hizo na kuwapiga makuhani hawa wa kichawi unakuwa umefanikiwa kuliondoa matatizo ya watu asilimia miamoja.

Mwanzo 4: 13 “Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.”

Tunaona alama inaanza kuonekana kwenye kitabu cha mwanzo kwenye Biblia. Tumeona Kaini amewekewa alama ili wale waliotaka kumuua wakimwona wasimuuwe sababu ya chapa aliyo nayo. Kwenye maisha ya watu.

Ufunuo 13: 16 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Mpinga kristo atatokea ambaye ni shetani ataamua kuvaa mwili. Haya yameandikwa tayari mwisho wa siku shetani hataweza kufanya kazi kwenye ulimwengu wa rohoni kwasababu watu wengi wanamshinda kwa kuomba na kufunga. shetani atahamia mwilini ili alindwe na sheria ya kibinadamu sababu huwezi kumuua binadamu mwenzako.

Hii itatokea baada ya unyakuo wa kanisa la Yesu Kristo. Maombi ya wakristo wa Ufalme wa Mungu ndiyo yanayokwamisha shughuli za shetani kwa asilimia miamoja. Baada ya Ufalme wa Mungu kuimeza dunia ndipo huyu mpinga kristo atakuja na chapa ambayo haitakuwa kwenye ulimwengu wa mwilini itakuwa inaonekana rohoni. Itakuwa mtu akienda kununua kitu dukani muuzaji akikuangalia atagundua huna chapa ya mpinga kristo kwa wakati huo hivyo hutaweza kununua wala kuuza sababu shetani atakuwa anatawala duniani.

Galatia 6: 17 “Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.”

Watu wa Mungu wanazo chapa za kristo na hizo zitusaidia kutokutaabishwa na awaye yeyote. Mpinga kristo amekwisha kuwepo duniani na kwamaana hiyo na chapa zake zipo zinawatesa watu.Kama ukishindwa biashara kariakoo hata ukihamia Mwanza utashindwa na huko sababu unazo chapa za kushindwa umewekewa. Mtume Paulo alivyosema mtu asimtaabishe sababu anazo chaapa za Kristo anatufundisha ukiwa na chapa za Yesu huwezi kutaabishwa.

Siku moja Yesu aliuliza chapa hii ni ya nani watu wakasema ni ya kaisari naye akasema ya kaisari apewe kaisari nay a Mungu apewe Mungu maana yake kama chapa uliyo nayo inahusu kutaabishwa basi utaabishwe, kama unayo chapa ya kuonewa basi uonewe, kama unayo chapa ya laana basi ulaaniwe, kama unayo chapa ya kuibiwa basi uibiwe. Na kama unayo chapa ya Mungu basi usitaabishwe upewe haki yako ya kufanya biashara na kufanikiwa, kustawi, kuzaa, kuoa, kusafiri, kuwa na afya njema, kuwa na utajiri na mali idumuyo sababu wamezibeba chapa za Yesu Kristo.
Kuna chapa za ukoo ambazo zimeshikia wana ukoo na kuwafanya mfano wasiweze kula mayai au wanakuwa na magonjwa ya kurithi, au wakioa au kuolewa lazima ndoa ziharibike au wanazaa nje ya ndoa au wana matatizo yanayofanana kizazi baada ya kizazi yote hii ni kwasababu wamewekewa chapa za kusababisha mambo hayo yawapate na hawawezi kukwepa mpaka chapa ziondolewe na ziwekwe chapa za Mungu kwa damu ya Yesu..

Mungu haikutosha kuwaambia wana wa Israeli kwamba wamepita katikati ya bahari ya shamu hivyo waendelee bali aliwaambia waweke chapa ili iwe kumbukumbu kwamba yeye ni Mungu anayeweza kugawa bahari sehemu yeyote na watu wake wakapita.
Wayahudi walifanya kila njia kwamba Yesu akafa na alipokuwa kaburini wakasema “Yule mwongo alipokuwa hai alisema atafufuka siku ya tatu sasa tuweke walinzi na wakamfuata pilato ili awape mhuri naye akawaambia nendeni mkaweke walinzi kama mtakavyo” 

Mathayo 27:66 "Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi."

Yesu alipokuwa kaburini waliweka walinzi kwa nguvu zote na wakatumia mhuri wa Ikulu ya Pilato wakapiga kwenye lile jiwe la kaburi ili mtu akigusa lile jiwe auwawe. Maana yake Yesu asitoke mle ndani ya kaburi. 

Unaweza kusafiri mpaka nje ya nchi lakini ukajikuta bado huwezi kutoka kwenye hali uliyo nayo, kuna chapa ya talaka kwenye ndoa, chapa ya umaskini, chapa ya kukataliwa unakuta mtu anazunguka kila mahali bila kupata mafanikio sababu amewekewa chapa ya kukaa ndani ya hali aliyonayo asitoke.

Kama kuna jambo ambalo shetani amefanikiwa kulidanganya kanisa la Yesu kuwaaminisha watu wakishaokoka basi kilakitu kinakuwa salama jambo ambalo sio sawa. Unakuta mtu anakwenda kanisani, anaabudu, anaomba, anatoa sadaka anaskiliza matangazo na kurudi nyumbani tena na tena. Huu ni uongo wa shetani ambao amewadanganya watu fikra zao ili wabakie kwenye vifungo alivyowafungia.

Ufunuo wa Yohana 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake”

Huyu shetani baada ya kuasi mbinguni alifukuzwa lakini hakutoka kirahisi bila vita kupiganwa ambayo alishindwa akashushwa mpaka hapa duniani. Kama shetani alikataa kutoka mbinguni mpaka ikapiganwa vita akapigwa na kutupwa mpaka kuzimu iweje leo ukae bila kupigana naye shetani na wakala zake hata kama umeokoka kutoka kwenye Ufalme wa giza ukaingia kwenye Ufalme wa Nuruni, huwezi kutoka kwenye kifungo cha chapa za kichawi kulichokufungia ndani ya umaskini, kuonewa, kukataliwa, talaka, kuharibu mimba, kutaabishwa na matatizo kwenye maisha yako bila kupigana.

Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani.”

Biblia inasema wakati malaika alishuka kwa kasi kutoka mbinguni akafika kwenye kaburi la Yesu uso wake ulikuwa kama umeme na wale walinzi kwa kumwogopa wakawa kama wafu. (kumbuka Malaika wawili tu ndiyo waliopiga miji ya Sodoma na Gomora yaani waligawana miji kila mmoja) umbo la asili ya malaika mmoja ni sawa na ghorofa 45 kwa mujibu wa kitabu cha Enoko mtu wa saba wa ukoo wa Ibrahimu.

Wakati hayo yanatokea Mathayo na wanafunzi wengine wa Yesu hakuwepo na hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya wale walinzi wa kaburi, maana yake wale walinzi ndio waliowaelezea nini kilichotoke. Ukisoma vizuri Biblia utaona imeishia kuelezea uso wake ulikuwa kama umeme akaliviringisha lile jiwe lililozuia mlango wa kaburi na kulikalia.

Mtu asikuambie kutoka kwenye hali uliyo nayo ni muujiza au ni mahubiri mazuri sababu kufanikiwa ni kuondoa mihuri ambayo umewekewa na inatakiwa iondolewe . Usishangae unazomewa nyumbani kwako na ukiamua kwenda kwingine unazomewa hivyo hivyo ni kwasababu ya chapa uliyo nayo inaruhusu kila unapokwenda uwe mtu wa kuzomewa tu. Mfano mzuri mtu akimwona nyoka lazima amkimbize ili amponde amuuwe sababu alishapewa alama ya kila atakaye mwona atamponda kichwa hivyo ni sawa na mtu ambaye amewekewa chapa za kukataliwa kila mahali atakapoenda atakuwa mtu wa kukataliwa tu.

Yesu alipotoka nje ya kaburi wanafunzi wake waliishia kusema alifufuka hawakusema alikuwa hivi au vile sababu Mungu akiondoa chapa kila mtu anakaa kimya na Yesu alipotoka alisema amepewa mamlaka yote mbinguni na Duniani na hapa tunajifunza kumbe unaweza ukawa na uwezo na nguvu kubwa sana lakini ukiwa umewekewa chapa huwezi kutoka kutumia nguvu zako.

Wachawi wanamashetani ya uchawi yanayowatambulisha kwa wacahwi wenzao na wakionana wanafahamiana. Kuna mashetani ambayo mtu akiwekewa hiyo inakuwa ndiyo alama au chapa(haionekani mwilini). Kuna wachawi wa alama nne:- wachawi wa kuzaliwa yaani mtu amezaliwa na mama yake alikuwa mchawi hivyo akamwachia urithi tangu akiwa tumboni, Unakuta mtu akizaliwa anakuwa na alama za uchawi na anakuwa mtu mbaya zaidi sababu ameupata tangu akwia tumboni mwa mama yake, Aina ya pili ni yule aliyezaliwa akapewa uchawi baada ya kuzaliwa, aina ya tatu ni uchawi wa kununua ambao mtu anaamua kuwakomoa watu na kuwaibia anaamua kununua uchawi, aina ya tatu ni uchawi wa kuwekewa ambao mtu anakuwa amefunikwa na uchawi bila ya yeye kujua.

KIRI
“Kwa damu ya Yesu alama yeyote ya kichawi iwe ni balaa au umaskini iliyowekwa tangu kuzaliwa kwenye maisha yangu naifuta kwa damu ya Yesu”

Alama ni mapepo ambayo yanatumwa kwa mtu na kumvaa ambayo wachawi wakiyaona sehemu yeyote wanakutupia matatizo kulingana na chapa uliyopewa mfano kama mtu anayo chapa ya magonjwa yanampata kwasababu ya chapa/mhuri aliowekewa. Kama mtu akiwa amewekewa chapa ya kufunga uelewa ukianza kuongea naye vitu vya maana utamwona ameanza kusinzia lakini ukimwekea mziki wa kidunia anaamka na kuanza na kuufurahia lakini ukimshauri vitu vya maana anaana kusinzia hakuelewi hii ni kwasababu mtu huyo amewekewa mhuri wa kutokuelewa. Kuna chapa zinazowafunga watu na zikifutwa na kuvaa chapa za Yesu kristo unapatikana ushindi asilimia miamoja.

1 Wathesalonike 2: 18 “Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.”
Zakaria 3: 1 “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.”

Ni kweli ukiwa umeokoka mapepo hayawezi kukaa ndani yako lakini yanafanya kazi nje yako. Mkono wa kuume maana yake ni eneo lako la nguvu mfano unataka kuomba kazi anamwingia mtoa kazi, ukitaka kupata visa anamwingia mtoa visa, ukitaka kufanya biashara anawaingia wateja hawaji kununua, ukitaka kufanya jambo fulani anakaa njiani kukuzuia usilifanikishe.

UKIRI
“kwa jina la Yesu nafuta kila Alana ya kichawi kwenye ukoo wangu, chapa za magonjwa, chapa za laana, chapa za mikosi nazifuta kwa jina la Yesu, nafuta chapa za kuharibu mimba, chapa za kuonewa nazifuta kwa jina la Yesu, chapa za uso nazifuta kwa jina la Yesu, nafuta alama zote za kifo kwa jina la Yesu nazifuta alama zote kwa jina la Yesu”

Kila kitu kina chapa yake, wa mbinguni na wa chini utaona kwa jinsi kinavyoonekana. Unaweza kumwona mtu anakufanyia kitu hata mwenyewe hajui kama anakufanyia jambo baya fahamu kuwa tatizo sio yule anayekufanyia mabaya bali ni chapa ya kuonewa na mambo ya kuonewa na kutokuwa na furaha yanakufuata popote uendapo sababu ya ile chapa uliyo nayo.

Yesu alipofufuka alikuwa nazo alama kwenye mwili wake japo ni Mungu lakini akikutokea anakuonyesha alama kwenye mwili wake ili ujue bado anaouwezo wa kukuokoa. Hakuna mtu ambaye ameumbwa na Mungu ili asifanikiwe kwenye maisha, uumbaji unatuonyesha tumeumbwa ili tufanikiwe na ukiona hujafanikiwa sehemu moja jaribu sehemu nyingine utafanikiwa. Kwasababu hii shetani na wakala wake wametengeneza mfumo wa kuwawekea watu alama ambazo kupitia alama hizo kama mtu amewekewa hizo alama hawezi kufanikiwa sababu alama zinamzuia usifanikiwe, unakuta mtu yupo kwenye ndoa lakini amewekewa chapa ya kuachika baada ya muda fulani nay eye hajui.

Umeumbwa ili ufanikiwe ukiona hufanikiwi ujue kuna kitu kimesimama mbele ya maisha yako, mwanamke amepewa uwezo wa kuzaa ukiona hafanikiwi kujifungua ujue amewekewa kitu kwenye tumbo lake asizae, ukiwa umewekewa mihuri hatakama unamtu wa kukusaidia hauwezi ukafanikiwa mpaka mihuri hiyo iondoke. Unaweza kumwona mtu anapambana kwa nguvu zote na hafanikiwi lakini akiamua kuondoa chapa hizo bila kuacha utashangaa kazi zinafunguka, biasahra inafunguka, ndoa iliyokuwa inakaribia talaka inaimarika, mimba zilizokuwa zinaharibika haziaribiki tena, Yule mtu aliyekuwa anakuchukia hakuchukii tena kwa jina la Yesu.

Wewe uko vile Biblia inavyosema na sio vile watu wanavyosema, uwezekano wa kufuta chapa zako ndiyo uwezekano wa kupata kazi unayoitaka, kufanya biashara unayoitaka utaifanya kwa jina la Yesu. Futa chapa za kichawi na uvae chapa za Yesu kristo uwe huru kwa Damu ya Yesu. Amen