RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UJUMBE: TAFSIRI YA ZINAA - MWALIMU MITIMINGI


Mwalimu Peter Mitimingi, akifundisha vijana katika semina kubwa iliyofanyika juzi kanisa la TAG Mwenge jijini Dar es salaam.



Tafsiri ya Zinaa:
1. Zinaa ni tabia yoyote ya kingono au inayompelekea mtu katika kufanya tendo la ndoa kinyume na makusudi ya Mungu juu ya tendo la ndoa.

2. Zinaa ni tendo au mawazo) ambayo yanapingana na viwango vya Mungu kuhusu tendo la ndoa.

3. Zinaa ni tendo lolote ambalo liko nje ya mpamgo na kusudi la Mungu la asili kuhusu tendo la ndoa.

1Koritho 6:18
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
• Inapotokea short ya moto umeme nyumba inawaka moto huwa unakimbia au unakimbilia kwenda kushangaa?
• Bomu linaporipuka huwa unakimbia mbali au unakimbilia karibu kuangalia?
• Zinaa ni kama short ya moto wa umeme kijana kimbia isije ikakuripukia.

Wimbo Ulio Bora 3:5
5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
• Mapenzi ni kama moto, usipochochewa hauwaki, bali ukichochewa unaweza ukawaka na kuunguza nyumba.