MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WAANDISHI WA HABARI WAKIVYOWEZA KUONGEA NA BISHOP DR.GERTRUDE RWAKATARE KATIKA HITIMISHO LA SEMINA YA MID-CROSSOVER SIKU YA JUMAPILI 03.07.2016

Hii ilikuwa ni siku maalumu ya kuliombea taifa la Tanzania na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Magufuli. Ibada hii ya maombezi ilifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 03.07.2016. Waandishi wa habari na watu mbalimbali waliweza kufika na kushuhudia jinsi Mungu anavyofanya mambo makuu katika ibada hii. Watumishi wa Mungu kutoka Arusha Bishop Danstani Maboya, kutoka Dodoma alikuwa Mch. Sylvanus Komba waliweza pia kuliombea Taifa la Tanzania na kumshukuru Mungu kwa kuvuka miezi sita na kuingia katika awamu ya pili ya kumaliza mwaka wa pili.
Bishop Dr. Getrude Rwakatare akiwa na waandishi wa habari osfini Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Ibada hii iliambatana na hitimisho la semina ya Crossover ambayo ilichukua muda wa siku 8 kuanzia 26.06.2016. Lengo la semina hili ilikuwa ni kujifunza Neno la Mungu, kumshukuru Mungu kufikia miezi sita, kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake na pia kumkabidhi Mungu atulinde katika awamu ya pili ya kumaliza mwaka tukiwa salama. Tunashukuru Mungu kwa siku hizo tatu kulikuwa na uhudhuriaji mzuri sana na watu waliweza kubarikiwa na mafundisho kutoka kwa Bisho Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Sylvanus Komba na Bishop Danstani Maboya.
Kanisa linawaombea waandishi wa habari kwa kazi yao nzuri na mwitikio wao mzuri wa kuweza kufika katika ibada hii maalumu. Mungu na azidi kuwalinda..ameni