MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

21.08.2016: MAMA ASHUHUDIA JINSI MUNGU ALIVYOMTETEA KATI YAKE NA NDUGU ZAKO JUU YA IMANI NA PIA ALIVYOWEZA KUMUOMBEA NDUGU YAKE NA KUPONA


Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa huruma zake anazofanya katika kanisa lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Watu wengi sana wamekuwa wakishuhudia jinsi Mungu anavyowatendea baada ya kufanyiwa maombezi na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (Mama wa Upendo). Mungu amekuwa mwaminifu sana na amekuwa akitekeleza kile alichowaahidia watoto wake.

Siku ya Jumapili 21.08.2016 mama mmoja aliweza kushuhudia Mungu jinsi alivyompigania katika mgongano wa kiimani na ndugu zake na jinsi Mungu alivyoweza kumtetea katika jaribu hilo na kumshangaza kwa muujiza wa kumponya ndugu yake. 

Tunaomba uzidi kufuatilia post zetu, kwani tupo katika maandalizi ya shuhuda hii.
Tunakualika katika TAMASHA LA MALOMBEZI ya Jumapili hii saa 3 asubuhi Mlima wa Moto Mikocheni "B", utaweza kuhubiriwa na mtoto wa miaka 5 Nice mwenye uwezo mkubwa sana wa kuijua Biblia, mahesabu ya sekondari, uimbaji, ualimu n.k. Mungu ana jambo na wewe...KARIBUNI SANA

 Mch. Prisca Charles (kulia) akiongea jambo na mama aliyeweza kushuhudia
 Kutoka kushoto ni Mch. Otieon, Mch. Prisca, Mhusika wa shuhuda na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (Mama wa Upendo)

 Mch. Noah Lukumay (kushoto)

 Mch. Fransis Mahichi (kulia) na Mch. Elizabeth Lucas (wa tatu kutoka kulia)