MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

ASEMAVYO MWAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA DAVID ROBERT

\Imekuwa kawaida yangu kulike post za almost kila rafiki alie kwenye page yangu and i real enjoy doing that. Kwa nini kwa sababu nafanya jambo ninalofahamu maana yake. Nataka nikwambie kwa nalike post picture zenu au zako kwa sababu ninakuheshimu sanaa kama Mungu mwenyewe kakuheshimu mimi nani nikudhalau au kukupuuza. Wewe ni mtu wa thamani sanaa na najisikia heshima na sifa kukufahamu na kuwa karibu nawe kupitia Facebook. Sijawahi kukuhukumu na sitakaa nikuhukumu kwa mavazi uliopost au maneno maana hiyo sio kazi yangu. Kazi yangu ni kukupenda, kukutia moyo, kujifunza kwako na ujifunze kwangu. Kazi ya hukumu ni ya Yeye aliekufia msalabani mimi sijawahi kumfia mtu hata mwenyewe siwezi kujifia na kujikomboa. Naamini nimezishinda dhambi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu aliye ndani yangu si kwa akili zangu wala uwezo wangu mwenyewe. Wala sikuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria ingekuwa hivyo nisingeokoka. Lakini ashukuliwe Mungu kwa rehema na Neema zake.

Nataka ujue wewe ni mtu wa thamani sanaa kwa sababu Bwana anakujua kwa jina maana amekuchora kwenye vitanga vya mikono yake ( viganja vya mikono yake). Hakuna mtu aliehukumiwa hadi sasa isipo kuwa mkuu wa hii dunia ( shetani) hujahukumiwa kwa sababu labda kesho utatubu kabla ya umahuti, labda utasikia neno litakubadirisha au labda utapitia magumu yatakayokusogeza karibu na Mungu mimi sijui kazi yangu ni kukupenda na kukuheshimu.

Chukua muda kutafakali juu ya ujumbe huu uliokujia asubuhi hii Bwana anasema na nafsi yako amua leo kumpa Yesu maisha yako upate faraja mafanikio, maisha ya ushindi, ufunguliwe katika uteka uwe uhuru leo Yesu anakupenda sanaa na hatauhukumu alimwengu mpaka wewe ufikiwe na habari hizi. Mungu akubariki NAKUPENDA