RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ASKOFU PENGO: VYOMBO VYA HABARI NI NGUZO MUHIMU KATIKA JAMII.

Askofu mkuu wa jimbo la Katoliki Muadhama Policarp Kardinali Pengo amevitaka vyombo vya habari nchini kutumika kuunganisha jamii ili kiwe kitu kimoja.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa miaka 20 ya utume wa Radio Maria Tanzania iliyofanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Spika wa bunge mstaafu Anna Makinda.

"Vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika ukuaji na ustawi wa jamii hivyo ni vyema vikajikita katika maudhui ya kujenga na kuleta umoja katika jamii", alisema Askofu Pengo

Aliongezea kwa kusema, "Hata tungedevelop Radio Maria kuwa television iwe ni ya kuunganisha baada ya kugawa tusiingize miziki ya kisasa ambayo wazee hatupendi kusikia vijana wanapenda kusikia," aliongeza.

Kulikuwa na risala iliyosomwa na Rais wa Radio Maria Tanzania, Humphrey Kira iliyotoa changamoto zinazo ikabili redio hiyo changamoto kubwa ya redio kuwa na ufinyu wa sehemu za usikivu yaani coverage area, pia ina vituo kumi tu vya kurushia matangazo licha ya kupokea maoni kutoka majimbo mbalimbali.

Askofu Pengo alitoa shukrani kwa wote waliohudhuria katika maadhimisho hayo na kutii mwaliko wa kuhudhuria katika siku hiyo. Katika maadhimisho hayo ya miako 20 ya utume wa Radio Maria, mwisho kulikuwa na harambee ya kuchangia redio hiyo ili iweze kujiendesha.