RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BASI LA KISASA ZAIDI LAZINDULIWA CHINA


MAFANIKIO ya Kiteknolojia yanazidi kupiga hatua sehemu mbalimbali duniani! Hii ni baada ya nchi ya China kuzingua basi la kipekee maarufu kama Transit Elevated Bus (TEB) lenye urefu wa mita mbili juu linaloruhusu magari ya kibinafsi kupitia mvunguni mwake limefanyiwa majaribio katika mji wa Hebei, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Basi hilo linalotumia umeme pia lina urefu wa mita 21 na upana wa futi 25, linategemewa kutatua kabisa tatizo la usafirishaji wa abiria katika miji yenye idadi kubwa ya watu, lina uwezo wa kubeba zaidi ya watu 300 .

Hii ndio mara ya kwanza kwa wabunifu kuonesha basi hilo hadharani baada ya video yake kuonekana katika mitandao ya kijamii mwezi Mei.

Tasmini iliyofanywa na watengenezaji wa basi hilo imeeleza kuwa, basi moja la TEB lina uwezo wa kubeba abiria wote katika mabasi 8 ya kawaida na linauwezo wa kuhudumu kwa kasi ya Kilomita 60 kwa saa na likiwa kwenye safai zake, gari zingine ndogo ndogo zinaweza kupita chini ya basi hilo bila kuleta madhara.

Takriban mabasi hayo manne yanawezwa kuunganishwa na hivyo kuwa na dereva mmoja.

Hivi ndivyo inavyoonekana

”Mabasi haya ni ya kipekee na moja ya faida yake kuu ni uwezo wake wa kubeba abiria wengi sana 300 kwa kila basi, pia itaokoa sana nafasi barabarani” alisema mhandisi mkuu katika mradi huo mpya wa usafiri Song Youzhou.

”Inahudumu kama vile treni za kisasa za umeme ila gharama ya kuwekeza kujenga njia na ukarabati barabarani ikiwemo ujenzi wa vituo maalum vya TEB ni 1/5 ”