RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": LAZIMA MUNGU AINGILIE KATI KATIKA MATATIZO YETU

Siku ya Jumapili Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwakumbusha waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni kuwa Mungu lazima aingilie kati mateso tunayopitia, alisema, "Leo ni tamasha la maombezi na uponyaji kwahiyo lazima tulisimike kwa maneno ya Mungu. Maneno ni Roho na hiyo Roho ndiyo inayoleta uponyaji. 
Tusome kitabu cha Yeremia 15:18, Neno la Mungu linasema, “Mbona maumivu yangu ni ya daima, jeraha yangu haina dawa, inakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe unakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?”, na hili ndilo Neno la Mungu. Yuko mtu ana ugonjwa sugu, yuko mtu ana tatizo la muda mrefu, anauliza kwa Mungu mbona maumivu yangu ni ya daima, majeraha yangu hayana dawa, yanakataa kuponywa, Mungu nifanye nini? Ni kweli wewe Mungu utakuwa huna masikio husikii? 
Mungu mbona ulisema kwa kupigwa kwake Yesu tumepona! Mbona mimi nimekili maandiko yote nab ado ninasikia maumivu? Mungu Neno lako litakuwa sio la kudumu, yaani ni kama maji ya mtoni lazima yapite? Huyu ni mwenzako. Pengine maneno haya si kwaajili ya mtu mmoja tu, bali kuna watu wengine walipitia majaribu mazito kwa muda mrefu, na sisi leo tunasema ni siku yako ya kufunguliwa, kuponywa. Pengine una ugonjwa unakutesa kwa muda mrefu, au tatizo linalokuandama kwa muda mrefu, tumesema lazima leo Mungu aingilie kati katika shida yako, au tatizo lako.

Bwana apewe sifa, ukiangalia sana yale mambo yanayotusonga mpaka kichwa kinazunguka. Unatakiwa kumuomba Mungu kuingilia kati na kusema, “Enough is Enough”, na sema nimechoshwa kupiga, “Mark Time”, ninasema hivi kwasababu Mungu lazima aangalie kwa matendo makuu. Mungu huwezi kumuona amevaa suti au kanzu anatembea bali Mungu utamuona kwa matendo yake makuu, hasa pale utakapovuka katika jaribu utasema huyu ni Bwana, utakapoinuka kiuchumi utasema huyu ni Bwana, utakapoona pesa ya ajabu utasema huyu ni Bwana. Ninachotaka kusema ni kwamba Bwana ameona mateso yako na anakwenda kukusaidia.