RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE NA MCH. NAOH LUKUMAY WAONGOZA IBADA YA KUVUNJA NIRA NA NGOME ZA SHETANI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Kama tulivyoambiwa kuwa Jumapili ya 14.08.2016 ni Jumapili ya kuvunja Ngome za Shetani, waamini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa hilo pamona na Mch. Noah Lukumay wakishirikiana na wachungaji na watumishi wa kanisa hilo waliweza kufanya maombezi ya kuvunja kazi za shetani na kumuomba Mungu aingilie kati kuwaokoa watu hawa ambao wamekuwa katika tope la mateso kwa muda mrefu sana. Hakika maombi haya yaliweza kufanya kazi kwani kuna watu walionekana kupiga makelele na wrengine kukimbia kanisani kutokana nammoto wa Yesu Kristo uliokuwa ukiuunguza kazi za shetani. Watu walitokwa na mapepo, majini na aina ya vifungo vyao. Mungu aliwaweka huru.

Ibada hii ilifabnyika barakja kwa walio wengi kutokana pia na uwepo wa Mungu uliokuwepo katika eneo la kanisa zima. Watu wengine waliweza kupokea Roho Mtakatifu na kuweza kunena kwa lugha wakimshukuru Mungu na kumshangilia kwa matendo makuu yaliyokuwa yakitokea katika ibada hii.

Inawezekana na wewe umefungwa katika mateso ya magoinjwa, madeni, kukosa ada au kodi, kushindwa masomo, magonjwa yamekuandama, umekosa kazi, huna kibali, huthaminiki katika jamii, umelaaniwa, umekosa ajira, umedhurumiwa, hupandishwi cheo kazini kwako n.k. tunakushi kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kupokea majibu yako. Uamuzi wako na imani yako ndivyo vitakusaidia wewe kupokea majibu yako. Amua sasa na ungana na wana Mlima wa Moto nao watakuongoza katika njia sahihi ya kupokea majibu yako.

Iambie nafsi yako inayokuambia usifike kanisani, iambie kuwa umeshindwa na kanisani utakwenda. Ukiona Roho fulani inakuzuia ujue inazuia njia zako za mafanikio. Watu wanafika katika kanisa hili wakiwa na imani, wakifuata yale Mungu anayotaka wafanye, na Mungu amekuwa mwaminifu kwao. 

Jitazame kwenye kioo na jiulize kwanini unapitia mapito magumu wakati watu wengine wanafurahia maisha yao na huku wanamtumikia Mungu....Kimbilia huku kwa Yesu....