TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE SIKU YA JUMAPILI 14.08.2016 ALIWEZA KUHUBIRI UJUMBE MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YETU

MAOMBI
Siku ya Jumapili 14.08.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwaombea watu wote waliofika katika ibada ya Kuziangamiza ngome za shetani Mlima wa Moto Mikocheni “B” akisema, “Pokea pesa kwa jina la Yesu, pokea dollar au pesa nyeupe kwa jina la Yesu, pokea safari za Ulaya kwa jina la Yesu. Yule Yesu mtenda miujiza yuko mahali hapa, yule Yesu aliyekausha bahari ya Shamu yuko mahali hapa, yule Yesu aliye mfufua Lazaro yuko mahali hapa,  yuko tayari kufufua kazi yako hautatoka kama ulivyo ingia. Mungu lazima akatende jambo jema kwako siku leo, ni siku yako ya kucheka, leo ni siku yako ya furaha utaondoka mwepesi kwa jina la Yesu.”


SAUTI ZA WATU WENYE SHIDA NI NYINGI, TUWASAIDIE
Mtu mmoja alikuja kwangu na kuniambia, "Mch. Bwana asifiwe  nina njaa sijala leo siku ya pili nina dozi ya UKIMWI ”. Dada huyu alikuwa na dozi ya UKIMWI anakunywa halafu ana siku ya pili hajala anasema, “Naomba nitumie hata Tshs. 10,000 tu walau nile chipsi dume chipsi dume (maana yake mihongo ya kukaanga)”, basi   palepale Roho wa Mungu akasema nami ili niweze kumsaidia huyu dada,  nikatuma Tsh. 10,000.

Baada ya kutuma meseji nikanijiubu, “Mchungaji asante nimepata,  nikitoka kula nitakupigia”. Baada ya kupata chakula na kula akanipigia akasema, “Mchungaji kitu ulicho nipa leo ni kama chakula cha mwezi mzima nimebarikiwa, nimefurahi nimekula chips na kuku na soda namshukuru Mungu kwa ajili yako”. Nachotaka kusema ni kwamba, sauti kama hizi ni nyingi watu wana matatizo, watu wengi wanashida, watu wengi wamevunjika moyo,  ni Mungu tu atakayeweza kuwaokoa, kuingilia kati akabadilisha hayo uliyonayo. Unachopata kumbuka kula na wenye uhitaji na usiwe mchoyo kwani Bwana hapendi kabisa na ni dhambi mbele za Mungu
TUHURUMIANE, TUCHUKULIANE NA TUSAIDIE
Iweni na huruma kwa watu wanaopita katika maisha magumu,  usifanye moyo kuwa mgumu bali  hurumianeni ninyi kwa ninyi. Yule ambaye hana chakula mpe chakula, ambaye hana nguo tafuta nguo nzuri mpe. Wamama mbarikiwe, wababa mbarikiwe, vijana mbarikiwe kwa kazi ya Bwana mnayoifanyakna ya kuwasaidia wenye uhitaji.

Mjukuu wa Bisho Dr. Gertrude Rwakatare

Tuchukuliane sisi kwa sisi katika shida zetu ili maombi yetu yasizuiliwe katika shida zetu.  Yupo Mungu mbele yako na katika taabu yako, zidi kuwa mvumilivu na kumtegemea. Mtu mmoja alinitumia meseji akasema,  “Mchungaji Nafanya sana kazi mimi naamka saa 9 usiku naelekea kazini, ninakaa kazini hadi saa 11 jioni, usafiri wa shida nafika nyumbani nimechoka,  ni miezi kadhaa sasa imepita watoto wangu hawajaniona,  wanasikia tu baba alikuwepo baba ametoka, lakini sina mafanikio katika maisha yangu, mchungaji naona nimefungwa, ninashida, sioni mbele nimekwama nashindwa kuona mbele wala nyuma.

 Naona mbele kuna giza na nyuma giza pembeeni giza. Mchungaji nifanyaje? Naomba niombee si kwamba mimi mvivu nafanyakazi sana mchungaji na siyo kwamba sijishughulishi,  najishuhurisha kama wanaume wengine lakini mpenyo siuoni nimefungwa.  Nikamuombea na Mungu akamfungua.


NAONGEA NA MTU ANAYEONA GIZA MBELE YAKE, HANA MSAADA WALE TEGEMEO.

Leo naongea na mtu anae ona giza mbele na nyuma,  hana msaada hana tegemeo leo Mungu ametupa  injili ya uzima. Kuna mtu mmoja ambaye amekuwa akiamka  saa 9 alfajiri anaenda kazini anarudi saa 11 jioni kila siku , anafika nyumbani amechoka na anakosa kukaa na watoto wake, analalamika akisema,  “Kazi hiyohiyo niliyonayo wenzangu wana magari, wamejenga, wamesafiri wamerudi, wanavaa vizuri lakini mimi kiatu kimechakaa”.

Leo ni wakati wa Bwana kujifunua kwako. Kuna watu wengi waliofungwa na wameshindwa kujenga na wamefanya kazi kubwa ila pesa wanayopata ni ya kula tu  “ Hand to Mouth”. Na huyu mtu anasema, “Hawezi kwenda kwa  mganga wa kienyeji kwasababu ameokoka”. Lakini leo “doctor” wa ma-“doctor “ Jesus Christ is here for you ”, Yesu yuko hapa kwa ajili yako lazima ufunguliwe.

Watumishi wa Mungu  tupo leo na vidonge vya kukusaidia ,  sindano yakukusaidia,  inuka leo Mungu akusaidie uinuke mahali ulipo, Mungu akutetea. Naongea na watu ndani ya nyumba ya Bwana yakuwa,  kufanya kazi isiyo kuwa na faida sio kiwango chako iliyeokoka.  Siyo kwamba hufanyi kazi unafanya lakini huoni pesa, huoni matunda, na unajiuliza kwanini?

Kama kuna mchawi alikufuatilia nyuma akachukua nyayo ulizo kanyaga akaenda kufunga mahali leo tuna mcheka kwani amejisumbua na atakiona na cha moto kwa Jina la Yesu Kristo. Pengine ulianika nguo yako ya ndani yeye akaona na akakata upindo wa nguo yako au gauni lako, tunakemea wabaya wako wote kwa Jina la Yesi Kristo aliye hai, na hicho walichokikata kikawarudie wao mara mia kwa Jina la Yesu Kristo.


WATU WATASHANGAA MAMBO YAKO YAKIANZA KUWA "SUPER"
Watu watashangaa watakapokuona unakuja na kichanga, watu watashangaa watasema huyu ni yeye au mwingine? Kwa kujiamini tunasema leo kwa shetani “enough is enough”,  Yeriko ilifungwa kwa ajili ya wana wa Israel walioteuliwa na hakuna aliyeingia ndani au  kutoka nje. Biashara unayoifanya wewe ni kubwa sana lakini kwa sababu umefungwa ndio maana huoni matunda. Umekuwa ukitoa  fungu la 10 lakini  bado hufiki mbali.

 Tunakufungua minyororo kwa jinla la Yesu Kristo. Yuko Mungu anaye fanya, unashida gani misukosuko gani? Umepita katika shida zipi? Yuko Mungu wa Mbinguni atakuinua si kwamba wewe huna sura nzuri ni kaka mzuri. Kuna dada mrembo mmoja alikuja ofisini na kusema, “Mchungaji hebu niangalie nilivyo mrembo, nina “shape” nzuri,   mguu wa chupa, nina mvuto lakini hakuna anayenichumbia mchungaji”.

Nikamjibu nikasea,  “Nimeuona mwenzangu”. Dada huyo akasema,  “hata murusi wa mwanaume kuniita hakuna. Mchungaji  unaona hata  nywele zangu  kama msomali,  nina shida usinione hivi napendeza. Mchungaji ninahitaji kuolewa,  umri unaenda,  nifanyaje mchungaji?”  Nikamwambia Mungu anasema, “Si vyema wewe kuishi bila mume wako, ukiona huna mume ujue huyo ni shetani amekufunga wewe msichana mzuri ndio maana huolewi.

Lazima tufungue ili usiwe mtu wa kusindikize wenzako.  Wewe utasindikiza harusi za watu mpaka lini?”  Umekuwa ukisema,  “Mchungaji nina shela sita za harusi za watu ila mimi si bibi harusi, sasa nahitaji kuitwa bibi harusi mchungaji”.  Nakutamkia  Fatuma Kandoro Mungu yupo Bwana ametakupa mume wako , wewe ni  msafi lakini huolewi.  Shetani amemfunga muwe wako usiweze kumuona. Kila mchawi aliyekuweka shela akakufunika mbele usionekane na wanaume leo tumelifungua shela kwa jina la Yesu, Mungu akusaidie katika jaribu lako.
 

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa na Mjukuu wake