RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

kipindi cha ujauzito ni moja ya vipindi vizuri sana kwa mama anayetarajia kupata mtoto, kipindi hiki hua na shida mbalimbali ambazo husababishwa na mabadiliko ya mama katika nyanja mbalimbali za mwili wake. kuna mambo ambayo ukisikia mama analalamika kipindi hiki ni kawaida lakini kuna mambo muhimu ambayo ukiyasikia kwa mama mjamzito basi lazima uchukue hatua kama ifuatavyo.

Kutokwa na damu sehemu za siri;
Damu nyingi kutoka sehemu za siri miezi mitatu ya kwanza ni dalili kwamba mimba imeharibika na kama damu hiyo inaambatana na maumivu makali ya tumbo la chini, inawezekana mimba imetungwa nje ya kizazi, lakini pia damu ikitoka kipindi cha miezi ya mwisho karibia na kujifungua ni dalili kwamba kondo la nyuma au placenta imejichomoa kwenye mfuko wa kizazi. hali hizi zinahiaji msaada wa haraka wa daktari hasa hasa mimba iliyotungwa nje ya kizazi, matibabu ya mimba iliyotungwa nje ya uzazi hua ni upasuaji wa haraka bila hivyo kifo huweza hutokea.

Kutocheza kwa mtoto:
kawaida mtoto huanza kucheza wiki ya 16 mpaka 25, kama mda huo ukipitiliza bila kusikia chochote au mtoto alikua ameshaanza kucheza baadae ukasikia kimya huu ni muda muafaka wa kuwahi kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi na matibabu huenda mtoto amefariki au ana tatizo fulani.

Kupata uchungu kabla ya wakati:

wanawake wengi hawajui tofauti ya uchungu wa kweli na ule ambao sio wa ukweli, mfano ukisikia maumivu kwa muda, maumivu hayo hayaongezeki na hayana muda maalumu huo sio uchungu. ila ukisikia maumivu yanayotofautiana angalau kwa dakika kumi na maumivu yanazidi muda unavyozidi kwenda huo ni uchungu wa kweli. wahi hospitali ukasaidiwe kujifungua au kama muda bado nenda hospitali ili wazuie uchungu huo ili mtoto asizaliwe kabla hajakomaa.

Kupasuka kwa chupa ya uzazi;
hii kitaalamu inaitwa rapture of membrane, halii hii hutokea muda fulani baada ya uchungu kuanza na ni kawaida, lakini ukiona maji yanamwagika ghafla na una mimba kubwa inawezekana chupa hiyo imepasuka hivyo kuhakikisha nenda chooni alafu kojoa mkojo wote, ukiona maji bado yanaendelea kutoka basi maki hayo yanatoka kwenye mfuko wa uzazi hivyo kimbilia hospitali haraka kwani mtoto yuko hatarini.

Maumivu makali ya kichwa, kutoona vizuri, tumbo kuuma na kuvimba miguu;
hizi ni dalili za kifafa cha mimba, ugonjwa huu umeua wanawake wengi sana kipindi cha kujiufungua, kuhakikisha hali hii nenda ukapimwe presha na ukiona presha iko juu kuliko kiwango cha kawaida wahi hospitali utibiwe.

Kichefuchefu na kutapika;
Ni kawaida kwa mjamzito kupata kichefuchefu na kutapika lakini hali hii ikizidi na mama kushindwa kula na kutapika sana huku akiishiwa nguvu basi akimbizwe hospitali illi aongezewe maji na kuatafutiwa chanzo cha tatizo.