RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EFATHA MWENGE: MCHUNGAJI: ADELLAILA LUIZA SOMO: MOYO WA SIFA

Mungu ni mwenye uweza haijalishi unapitia katika kitu gani iwe ni maumivu ya aina gani furahi maana anakupenda, unatakiwa ufurahi maana hii ni moja ya shukrani yako kwake. Filipi 4:4 “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. ” Unapofurahi unasukuma magonjwa mbali na wewe na adui yako anakimbia mbele yako. Kufurahi kwako siku zote adui yako anakuwa mdogo kuliko sisimizi, unapokuwa na huzuni adi yako ndio anafurahi bali furaha ya Mungu ni kukuona unafurahi.
 UTAMJUAJE MTU MWENYE MOYO WA SIFA AU WA SHUKRANI 1. Anakuwa na furaha wakati wote, mtu wa aina hii siyo kwamba hana ambayo anayopita nayo hapana lakini ana moyo wa shukrani mbele za Mungu, ukifurahi mbele za Mungu hatakama unamagonjwa yanaponywa na furaha yako itakufanya uwe na Mungu kila wakati. 2. Mtu mwenye moyo wa sifa anakuwa na shukrani, Mungu akiona una moyo wa shukrani anakupa kila kitu unacho kihitaji. 3. Mtu mwenye moyo wa shukrani anakuwa na UPENDO wa kujipenda mwenyewe na wakupenda wengine. 1korintho 13:4-8 “Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;……….. ” mtu anayependa wengine hawezi kuwaona wanalia halafu akanyamaza balia anawahurumia na kuwasaidia. 4. Mtu mwenye moyo wa sifa wakati wote anasimulia matendo ya Mungu, 5. Mtu mwenye moyo wa sifa hana manung’uniko wakati wote anashukuru katika kila jambo.


Kwaya ya vijana waimbaji chipkizi Efatha wakiongoza Ibada ya tatu kumsifu na kumuabudu MUNGU. Hakika SIFA NA UTUKUFU zina MUNGU.





KILA JAMBO NA WAKATI WAKE. Leo ni siku muhimu sana kwa ndugu zetu hawa, ambao leo wameamua kuyatoa maisha yao kwa BWANA YESU ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yao. NEEMA ya MUNGU iwe nanyi iwatunze asiwepo atayerudi nyuma. MTAKUWA WATU WAKUU, Wengi wataokolewa kupitia ninyi.




PICHANI: Mama Eliyakunda Mwingira akisalimia kanisa katika Ibada ya kwanza na kutoa salamu kutoka kwa Baba yetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, ambaye yupo mikoani katika kuifanya kazi ya Mungu.
\
MCH. FRIDA MNYANGI SOMO : NGUVU YA UPENDO Mungu ni pendo ukiwa na nguvu ya upendo inasababisha kuwa na huruma huta mkanyaga jirani (Yohana 3:16-17 " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.") Japo tulikuwa na dhambi, MUNGU alitusamehe hata kabla ya kumwomba, na sisi tunatakiwa kuwasamehe waliotukosea hata kama hawajaomba msamaha. Upendo unaanzia kwa mkeo ama Mumeo na kwa watoto na kwajirani yako kwani hainamaana kwamba unampenda Mungu wakati Mumeo mkeo humpendi. Hata kama jirani yako amekusengenya mpende tu usimshikilie mtu ndani ya moyo wako, Hata ukinenewa mabaya potezea futa kabisa ili uweze kuiona mbingu. Ukimpenda Mungu lazima umpende na jirani yako aliye umbwa kwa sura ya Mungu (1Yohana 4:19-20 "Mtu akisema anampenda Mungu naye akimchukia ndugu yake ni mwongo, asiye mpenda ndugu yake ambaye hakumuona hawezi kumpenda Mungu asiye Mwona"). - Nguvu ya upendo inasabababisha unakuwa na msamaha - Inasababisha kumpenda mtu hata kama anakufanyia mabaya ikiwa ndani yako utamsamehe bila yeye kuomba msamaha

PICHANI: Efatha Mass choir wakimsifu na kumwabudu MUNGU WETU MKUU kwenye Ibada ya pili inayoendelea hapa Efatha Mwenge Dar es salaam



Mchungaji Margareth Ilomo: WAOMBEE WANAOKUUDHI ILI UWE MKAMILIFU: Ukiwaombea wanaokuudhi na kuwatangazia msamaha ni injili tosha, Mtu akikuudhi nenda kamnunulie zawadi nzuri na umpelekee, ile zawadi itamfanya akupende na wakati mwingine atakutete akisikia mtu anakusema vibaya atasema yule hapana hayuko hivyo. Je ulisha wahi kumnunulia zawadi mtu aliyekuudhi? Fanya hivyo na utamwona MUNGU katika maisha yako. 2 Timotheo 3:12 "Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa, lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika."å