Select Menu

News

USIKOSE IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

USIKOSE IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

MLIMA WA MOTO JUMAPILI HII

MLIMA WA MOTO JUMAPILI HII

SARAH KUZINDUA ALBAM YAKE JUMAPILI HII

SARAH KUZINDUA ALBAM YAKE JUMAPILI HII

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» » HABARI ZA PASTOR DONNIE MCCLURKIN KUVALISHA MCHUMBA PETE BADO KITENDAWILI


Sanga Rulea 11:39 AM 0Moja ya habari kubwa zilizosambaa kwa wapenzi wa muziki injili duniani mwishoni mwa wiki iliyopita ni matukio mawili makubwa kutoka kwa waimbaji nguli wa muziki wa injili mchungaji Donnie McClurkin kumvalisha pete ya uchumba mwimbaji mwenzake Nicole Mullen habari iliyoenda sambamba na picha ya wapendwa hao, habari ya pili ni mwimbaji Israel Houghton nayeye kumvalisha pete ya uchumba mwanadada maarufu mtangazaji wa runinga aitwaye Adrienne Bailon huko jijini Paris nchini Ufaransa.

Israel na mchumba wake


Wakati watu wakiwa bado na furaha huku waimbaji wengine maarufu kama Fred Hammond wakipongeza hatua ya waimbaji wenzao, jioni ya jana mwimbaji mwingine mwanamama Erica Campbell aliyeamua kukanusha kwamba si kweli kwamba Donnie na Nicole wamevishana pete ya uchumba na kuwataka watu kuupuuza mtandao wa Christian Post kwakuwa wamebadili ujumbe wa mchungaji Donnie alipozungumza kwenye kipindi wiki iliyopita ambapo watu wanasema ni kweli mchungaji huyo alidai kuwa yupo mbioni kufunga ndoa lakini hakusema kama amevisha mtu pete.

Kutokana na kuwepo kwa taarifa hizo, huku wahusika mpaka sasa wakiwa wamekaa kimya, imembidi mwimbaji mwingine aliyewapongeza Yolanda Adams akanushe pongezi zake na kusema kwamba bado watumishi hao wapo vizuri kabisa, ila taarifa za kuvishana kwao pete ya uchumba ni heri kusubiri watoe tamko, ambapo ilibidi aombe radhi kwa kitendo hicho. 

Picha ya mkono wa Adrienne mchumba wa Israel ukiwa na peteAidha kwa upande mwingine tukio la mwimbaji Israel Houghton kumvisha pete mtangazaji huyo kumepokelewa kwa namna tofauti na mashabiki wake na wapenzi wa gospel hasa baada ya mwimbaji huyo kutenda kitendo hicho wakati alishaoa kwa ndoa na kutalikiana na mkewe mapema mwaka huu, wakihoji yeye kama kioo ni kwanini afanye kitu kama hicho?Huku baadhi yao wakidai msichana ambaye alihusika katika kuharibu ndoa ya mwimbaji huyo baada ya kufanya uzinzi ndiye aliyevishwa pete na mwimbaji huyo.


å


Source: GOSPEL KITAA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS