TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

KOFU MTOKAMBALI ACHAGULIWA KWA KISHINDO KULIONGOZA KANISA LA TAG KWA AWAMU NYINGINE

Askofu Mkuu wa T.A.G Dkt Barnabas Mtokambali
Askofu Dkt Barnabas Mtokambali amechaguliwa kwa kishindo kuwa askofu mkuu tena wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) katika mkutano mkuu wa kanisa hilo unaofanyika mkoani Dodoma. Askofu Mtokambali amepata jumla ya kura 2250 kati ya kura zote zilizopigwa 2403 huku aliyemfuatia askofu Dkt Lawrence Kametta amepata kura 128.

 Aidha kwa upande wa makamu wa askofu Magnus Muhiche amechaguliwa kushika wadhifa huo, huku kwa upande wa katibu mkuu ikikamatwa na Rony Swai
Askofu Mtokambali mkutanoni Dodoma

Maaskofu na Wachungaji wa TAG wakimpongeza Askofu Mtokambali baada ya kutangazwa mshindi

Viongozi waliochaguliwa wa kanisa la TAG
Hali ilivyo mjini Dodoma kwenye mkutano wa T.A.G