MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MANENO YA BUSARA KUTOKA KWA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA PAUL CLEMENT

Palikuwa na ndugu mmoja anaitwa Obedi yeye alikuwa ni mtumwa kwa watu fulani na alikuwa mtumwa sababu kijiji chao kilivamiwa na watu fulani waliojulikana kwa jina la Waamili Hawa waamili walikuwa wanavamia vijiji mbali mbali na huuwa watu na kuchukua vijana wenye nguvu na kwenda kuwauza kwa wafalme huku wao hao waamili walikuwa wakipata dhahabu baada ya kuwauza hao vijana na huyu Obedi alikuwa mmoja kati ya watu ambao kijiji chao kilivamiwa watoto na wazee waliuwawa. vijana zaidi ya arobaini walichukuliwa katika kijiji chao na Obedi alikuwa mmoja kati ya vijana hao.


Safari ilianza kwenda katika mji Abiga ambao ulijulikana kwa jina la Mji wa bidhaaa bidhaa hizo walikuwa ni watu wakike na wakiume na mji huo wa Abiga ulikuwa ni mji mkubwa sana uliojengwa dhahabu na majengo yake yalikuwa mazuri sana hivyo wafalme walitembelea sana mji huo kununua watumwa vijana wenye nguvu na pia kutafuta masuria (wanawake).Pia mamalkia wengi walitembelea mji huo kununua vijana wenye nguvu ili wqwatosheleze na kununu vijakazi. Hivyo safari ya kwenda Abiga ilikuwa ndefu sana huku wakina Obedi waliwa wamefungwa minyororo huku wakipigwa na mijeredi kama punda wengine walifia njiani lakini wengine walipona akiwemo Obedi basi walifika mpaka mji wa Abiga wakati wanaingia waliona mji ulivyokuwa mkubwa walishangaa mwenzake obedi alimwambia obedi "obedi kuwa mtumwa katika mji huu ni raha ona jinsi mji huu ulivyokuwa mkubwa na mzuri" obedi alimuangalia mwenzake kwa hasira kisha akamjibu "acha ujinga wewe pamoja na mji huu kuwa mzuri na kujengwa kwa dhahabu lakini bado hauwezi fanana na thamani ya ndugu waliouwawa kikatili na watu hawa wala hauwezi fanana na thamani ya wazazi wangu na wadogo zangu waliuwawa na watu wa mji huu hivyo basi sifurahii kuwa mtumwa katika mji huu ila nitafurahia nikiungusha mji na ufalme wake".walifika mpaka eneo la mauzo ya watu Obedi alipandishwa sehemu ya juu ambapo kila mtu anamuona na wafalme wengi kutoka miji mbali mbali walikuwa wamefika hapo kununua watumwa na walipomuona Obedi na jinsi alivyokuwa na mwili mdogo walimdharau wakasema mtoeni hapo mlete mwingine na Obdedi akashushwa akapelekwa mahaka pabaya ambapo watu hutumikishwa kwa kazi ngumu za kubeba mawe na kujenga miji Obedi alipelekwa huko na akaanza kufanya kazi huko alifanya kazi huko mwaka mzima na sababu walikuwa wakimaiiza kufanya kazi wanafungiwa katika magereza baada ya mwaka Obedi mwili wake ulikuwa umejijenga sana na ukawa mkubwa sana wenye nguvu sana.


Siku moja Mfalme wa Abiga alitembelea eneo hilo akamuona Obedi akifanya kazi hakumtambua kuwa ni yule waliyemkataa siku ya mnada sababu alikuwa na ndevu nyingi kidevuni na nywele nyingi kichwani na mwili wake ulikuwa umejaa sana na alikuwa na misuli katika mapaja yake na katika mwili wake wote Mfalme alipomuona aliagiza akisema "nileteeni huyu kijana katika ufalme wangu" walimpeleka Obedi katika baraza la mfalme Mfalme aliamuru Obedi apelekwe kwenye mafunzo ya askari awe mmoja wa askari wake Obedi alipelekwa katika mafunzo na huko mafunzoni alikuwa ni askari bora anayeweza kutumia panga vizuri mkuki na upinde vizuri na alikuwa na uwezo wa kuuwa wanajeshi mia wenye siraha kwa kutumia kisu kidogo na baada ya hayo mfalme alimteuwa obedi kuwa juu ya askari wote yani yeye ndio mtoa amri.siku moja mshika kikombe cha mfalme alimfuata obedi na kumwambia ni heshima kuwa mtumwa katika nyumba ya mfalme" obedi akamuangalia kwa hasira kisha akamwambia "kuwa mtumwa ni sawa sawa kuwa mbwa Katika anayekula makombo kwa bwana wake" kisha akaondoka siku moja mfalme aliandaa sherehe kubwa na akawaita wafalme wenzake wengi washerekehe na siku hiyo Obedi alikuwa amepanga ndio siku ya kuiangusha Abiga maana nia yake ni kulipa kisasi kwa mji wa Abiga na ufalme wake sasa wakati mfalme akiendelea na sherehe Obedi aliuwa askari wote wa Abiga huku Mfalme hajui kinachoendelea sasa mfalme akiwa amesimama akizungumza ghafla mkuki ulimuingia kifuani alidondoka chini kufa kisha obedi alikuja mpaka pale aliposimama mfalme kisha akasema "kuanzia sasa hakuna utumwa tena watu wote waliochukuliwa katika miji yao wakitaka kurudi kwao warudi kwa ndugu zao na wote hakuna utumwa tena na wafalme waliokuwa pale waliwekwa chini ya ulinzi wakaambiwa andikeni barua katika miji yenu ya kuwaacha huru watumwa wote wakafanya hivyo na watu wakawa huru wote.na hao watu waliposikia aliyoyafanya Obedi walimtaka awe Mfalme katika mji wa Abiga na kweli Obedi akawa mfalme katika mji wa Abiga.
Jeh! Umejifunza nini kuhusiana na hii story fupi?