RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Mch. MAMA MGETHA: HAKUNA JAMBO BWANA ASILOLIWEZA

Mch. Mama Mgeta

Siku ya tamasha la maombi na kuvunja ngome za shetani katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”, mch. Mama Mgeta alikuwa na haya ya kusema, “Bwana Yesu asifiwe. Naomba usome kitabu cha Yeremia 32. Leo hii tumeambiwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuwa siku ya Jumapili ya tarehe 31.07.2016, kuna tamasha la maombezi ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Tumezoea kusikia matamasha ya waimbaji lakini tunamshukuru Mungu kwa kumpa maono mtumishi wa Mungu kuwa leo hii tuwe na tamasha la maombi. Kama watumishi wa Mungu tunahitaji maombi na kwa wote wenye mwili. Unatakiwa kujiuliza Je, kuna jambo ambalo Mungu asiloliweza? Yawezekana umeenda mahali fulani kama vile hospitalini kupimwa ugonjwa wako, na ukaambiwa ugonjwa wako hauna dawa. Unatakiwa kutambua kuwa hizo ni akili za daktari ambaye ni mwanadamu tu tunayempenda. Lakini unatakiwa kujua kuwa kuna daktari wa madaktari ambaye ni Yesu Kristo mwana wa Mungu ambaye anakuja kwako kwa njia ya swali anasema, “Mimi ni Mungu wa wote wenye mwili, Je, Kuna jambo nisiloliweza?” Yaliyoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana. Mimi kama Mama Mgetha kuishi kwangu ni muujiza, kwani miaka ya nyuma, niliumwa ziwa na kupasuliwa mara tatu, lakini madaktari wakasema, “Hatuoni kitu”. Nilipokata rufaa kwa Bwana, na Bwana aliniponya, kwa maana hakuna jambo Mungu asiloliweza.

Yako mambo ambayo umefika mwisho wa akili zako, lakini siku ya leo Bwana anasema, “hakuna jambo asiloliweza”. Ukifika mahali ukaona umefika mwisho, ujue hapo ndipo Bwana anapoanza. Kuna kipindi fedha yako mwenyewe itashindwa kukusaidia lakini jina la Yesu linaweza kukusaidia. Ninakumbuka nilipokuwa India, mume wangu akiwa amezingilwa na mitambo ya mashine hospitalini, nikajikunja mahali kwenye kochi (nimekunja miguu), wakati akaunti ya mume wangu benki ina pesa ya kutosha. Lakini zile pesa hazikumsaidia chochote tukawa tunateseka, ikabidi nipige simu kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anisaidie naye akatuombea. Kuna wakati degree haikusaidii chchote wala kisomo chako bali Jina la Yesu ndio msaada wako wakati wa shida. Hakuna jambo Mungu asiloliweza kwa hilo lililokuuumiza, Mungu yupo hapa Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Umelia imetosha mpendwa, umeomboleza imetosha mpendwa, na ndio maana Mungu anakuja kwako kwa njia ya swali. Mungu anakuuliza, mbona nimekupa macho mawili, masikio mawili, nimekupa mikono na uanatakiwa kujiuliza ni nani awezaye kuumba viungo. Unaweza ukawa unaumwa na hujui ni nani ana “spear” zako, sasa nataka kukuambia aliyekuumba ana “spear” zako. Unatakiwa kumwambia Jehova kuwa hii damu yangu yenye malaria, yenye typhoid sihitaji tena bali ninahitaji damu ya samba wa Yuda (Yesu) aliyekufa msalabani, damu ya Yesu haina virus vya malaria.