MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MFUNDISHE MWANAOMAMBO HAYA YA MSINGI YATAKOYO MSAIDIA MAISHANI MWAKE
Ni familia chache sana ambazo zimekuwa zikiwafundisha ujuzi huu watoto wao na hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri ya mafanikio huku familia nyingi hasa za wasomi zikiwasisitizia watoto wao elimu tu kama ndio njia kuu ya kufanikiwa kimaisha.

Elimu ya stadi za maisha kwa watoto na vijana hutofautiana kulingana na umri na eneo mnaloishi. Hivyo mafunzo haya yasingatie hivyo vigezo mbili

Kama unamtakia mtoto/kijana wako maisha bora na yenye mafanikio ya baadaye mfundishe au muelekeze stadi za maisha zifuatazo:

1. Mfundishe mwanao namna ya kuandaa bajeti ya pale nyumbani kwako kwa kutumia karatasi na au kompyuta

2. Mzoeshe mwanao kulipa bili mbali mbali kama za TV, tanesco, maji nk

3. Mzoeshe mwanao kufanya manunuzi sokoni na supermarket

4. Mzoeshe mwanao kurekebisha/kutatua matatizo madogomadogo ya pale nyumbani kama ya umeme, maji, TV, vitasa vya nyumba, rangi, nk

5. Nenda naye kazini kwako hasa wakati wa likizo na kumfundisha kazi zako taratibu kama fursa inaruhusu mfano namna ya kupiga simu za kiofisi, namna ya kuandika na kutuma email, namna ya kutuma na kupokea faksi, namna ya kuprint na kutoa photocopy, namna ya kuscan, namna ya kuafail na kutoa barua kwenye mafail (badala ya kumpeleka tuition)

6. Mzoeshe utoaji mfano kanisani mpe sadaka akatoe yeye kwa niaba yako au mpe sadaka kama yako. wewe ukitoa 5,000 na yeye mpe elfu tano kama huna basi wewe baki mpe mtoto akatoe kwa niaba yako. Mzoeshe pia kutoa kwa maskini na wenye uhitaji.

7. Usimzoeshe mtoto kutoa sadaka za kitoto kama mia moja nk. Atazoea kutoa kidonjo hata akiwa mkubwa.

8. Mzoeshe kuwaombea wadogo zake, wakubwa zake, majirani, eneo mnaloishi, nchi, viongozi, marafiki na maadui kama wapo.

9. Mfundishe na umzoeshe kufanya biashara ndogo ndogo pale nyumbani (kulingana na umri wake)

10. Mzoeshe kuongoza ibada ya nyumbani na kufanya maombi

11. Mzoeshe kwenda kusalimia marafiki na majirani wa karibu (close friends and relatives)

12. Mzoeshe mwanao pia kuwatembelea watu walio kwenye shida mfano kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, wafungwa magerezani na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwenye vituo vya kulelea watoto yatima nk.

13. Mzoeshe kusema samahani anapokosea na asante anapofanyiwa wema na kusema nimekusamehe anapoombwa msamaha

14. Mzoeshe kusifia mwenzake hasa wadogo zake au wakubwa zake pale wanapofanya vizuri hata kama ni kwa haba

15. Mzoeshe kuwa mdadisi wa mambo (critical thinker) Mfano kwani ukirusha kitu juu inarudi chini, kwa nini mchana kuna mwanga na usiku kuna giza? kwa nini tunakula? kwa nini anasoma? na maswali mengi ya kimaisha

16. Mzoeshe mtoto wako kufanya jambo jipya kila siku au jambo lilelile kwa namna mpya (to be creative and innovative)

17. Mzoeshe mtoto kusoma (mfano vitabu, magazeti, majarida yenye kuelimisha)

18. Mzoeshe mtoto kutambua vipawa na vitu anavyovipenda kufanya ili aviendeleze

19. Mzoeshe mtoto kupenda wenzake kwa matendo. (mfano kumwomba Mungu amuwezeshe kupenda wengine, kuwaombea wengine wapate mafanikio kwa Mungu, kuwapa zawadi wadogo zake na wakubwa zake -akinuanua pipi mbili, moja yake na moja ya rafiki yake au mdogo wake au mkubwa wake)

20. Mfundishe mtoto wako mambo kadha wa kadha ya kimaisha kama vile uongozi, usimamizi wa fedha, biashara na ujasiriamali, namna ya kufanikiwa katika masomo, namna ya kuweka vipaumbele, namna ya kuhusiana na wenzake, namna ya kutatua migogoro yanapotokea, namna ya kufanya maamuzi hasa maamuzi magumu. nk

21. Jizoeshe kutoka out kama za lunch, kutembea, shopping na mtoto wako na kutumia huo muda kumfundisha mambo kadha kadha ya kimaisha. Hii inategemea out hiyo ni ya wapi na ya kusudi lipi. Utakachomfundisha mtoto wako kiendane na mazingira yaani out destination na umri wake

22. Jizoeshe kupumzika na mtoto wako na kufanya yale mambo mtoto anafanya (mfano kuangalia TV pamoja, kuangalia mechi za mpira pamoja, kucheza nk. kwenda kutembea pamoja ili uweze kumjua mtoto wako na anapendelea mambo gani na pia upate fursa ya kumuelekeza kwenye mambo yanayofaa zaidi). Tumia pia muda huu kumfundisha mtoto wako mambo kadha wa kadha ya kimaisha

23. Jizoeshe kumkumbatia mtoto wako hasa mnaposalimiana au kushangilia jambo, au unapoelezea hisia zako za furaha kwake ili uimarishe mahusiano yako kwake na pia ujue kama yuko salama ili pale anapokuwa sio salama uwe wa kwanza kumtambua na kuonyesha upendo wako kwake kwa kumhudumia na kumpa maneno ya faraja. 

Watoto wengi wana tabia ya kuficha matatizo walizo nazo kama wazazi hawako karibu nao, mfano ana kidonda, ametendewa mabaya na wenzake au watu wabaya, ugonjwa wa ngozi, na magonjwa mengine.

24. Unapokuwa na mazoea ya kumkumbatia mtoto wako utagundua mambo hayo. Mfano, kwenye kijiji kimoja hapo mwaka 1998 tulimtembelea mtoto mmoja katika na katika hali ile ya kumkumabtia tukagundua kuwa aliungua mgongoni na kwa hiyo tukafanya utaratibu wa haraka wa kumpeleka kwenye zahanati ya karibu akatibiwe kidonda kwani kilianza kuoza. Mfano mwingine:

Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa tangu utoto wake hakuwahi kuwa karibu na baba yake kwani alikuwa mkali sana na siku moja walikubaliana na mama kumpiga kwa kosa ambalo hakulitenda. Kuanzia hapo akawa mbali na wazazi wake mpaka alipohitimu chuo kikuu.

25. Hata adhabu tunazowapa watoto ziwe za kistaarabu. mfano umshirikishe mtoto kwenye adhabu yeyote unayotaka kumpa. Umsikilize vya kutosha kabla ya kumpa adhabu yeyote. Hata kama adhabu ni kali, mtoto akishirikishwa na kuridhika kwamba alistahili kuadhibiwa hataweka uhusiano wake na mzazi mbali.

26. Fanya matukio kama ya birthday pamoja na mtoto wako huku akiwaalika marafiki zake wa karibu (hii itakuwa fursa yako ya kuwafahamu marafiki wa mtoto wako) mfano waweza weka kwenye electronik kalenda yako ikukumbushe birthday za watoto wako ili wewe ndie uwe mkumbushaji na kuhakikisha tukio hilo linafanyika. Kumbuka aina ya marafiki wa mtoto wako ndio watakaoamua mtoto wako aweje mbeleni na afanikiweje? awe na tabia za namna gani? nk

27. Mzoeshe mtoto ajifunze kuwasikiliza wengine kwanza sio yeye tu asikilizwe tena kwa kumwangalia msemaji usoni na kujifunza kutumia luigha ya mwili kuwasiliana.

28. Unapombeba mtoto wako kwenye gari muelekeze mambo kadha wa kadha mfano kuwasha gari, kuzima, kushika mbreki, kutumia usukani nk)

29. Mzoeshe mtoto kuweka kumbukumbu kwa kuandika na jinsi ya kutunza mafaili yake kwa mpangilio sahihi, mfano matokeo yake yawe kwenye faili la kwake ambalo yeye mwenye analisimamia.

30. Mzoeshe mtoto namna ya kutengeneza ratiba na kuifuata mfano ratiba ya siku, kuamaka, kufanya usafi, kwenda shule, kujisomea, kufanya homework, kufanya kazi za nyumbani, kucheza kuangalia vipindi maalum za TV au kanda nk.

31. Mtoto ajizoeshe kuandika maono na malengo ya maisha yake ya muda mfupi, kati na mrefu

32. Mzoeshe mtoto kutumia usafiri wa umma kama daladala.

33. Mzoeshe mtoto kuwasiliana naye kwa barua ili azoee kuandika barua nzuri mfano za maombi ya vitu vinavyotakiwa shuleni na bei yake.

34. Mzoeshe pia mtoto kufanya window shopping kwa vitu vya shuleni
na zile za nyumbani kama vyakula na vifaa vingine vya nyumbani ili ajifunze naman ya kufanya manunuzi kwa dhamani halisi ya pesa (value for money).

35. Mzoeshe mtoto kutumia kompyuta kwa matumizi madogomadogo kama ya kuanda bajeti kwa excel na kuandika maombi kwa MS Word

36. Mzoeshe mtoto kuogelea hasa kwa wale walio karibu na mito, maziwa na bahari

37. Kama hali ikiruhusu fanya utalii wa ndani na mtoto wako kama kutembelea mbuga za wanyama (kwa walio karibu na mbuga hizo) kutembelea matukio ya kimila, kutembelea zoo ya wanyama nk.

38. Mnunulie mtoto kamera ndogo ya kujifunzia na awe anatumia kwenye matukio muhimu makanisani, shuleni nk

39. Mzoeshe mtoto kutumia vifaa vya teknolojia kama simu an kompyuta katika kuwasiliana kwa message, email na sauti

40. Mambo haya hayawezekani ndani ya muda mfupi. inategemea pia na umri wa mtoto wako na mahali mnapoishi.

Vipengele vingine havihusiki na wewe kulingana na mazingira yako ya kuishi na umri wa mtoto wako

Pia kuna mambo mengi katika maisha mfundishe mwanao asijihusishe nayo kabla ya wakati wake. mfano mitandao ya kijamii, makundi ya marafiki wasiofaa/wasiojenga maadili, ulevi, mahusiano ya kingono au kimapenzinkBy Richard Edward å