RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MRISHO GAMBO ATEULIWA KUWA RC MPYA ARUSHA

Mkuu Mpya wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi wake na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).

Uteuzi wa Gambo unakuja takriban miezi miwili baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha mwisho mwa Juni mwaka huu.
Felix Ntibenda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyetenguliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.