RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MZEE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B", LILIAN MWAKITALU AMSHUKURU MUNGU KWA UPONAYAJI BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI NCHINI INDIA

Siku ya Jumapili ya tamasha la Maombezi na kuvunja ngome za shetani 31.07.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar es Salaam, kwa Dr. Gertrude Rwakatare, Mzee Mwakitalu na mke wake Lilian Kitalu waliweza kumshukuru Mungu kwa uponyaji baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo kwa Liliana Mwakitalu. Mzee Mwakitalu alikuwa na haya ya kusema, “Kanisa la Mungu, Bwana Yesu asifiwe sana. Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwaajili ya neema hii ambayo ametupa kuweza kukusanyika nyumbani kwake. Asante Askofu wangu Dr. Gertrude Rwakatare kwa maono haya ambayo hata Mungu mwenyewe akakupa kundi hili kubwa la watu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. 
Wapendwa kuna siku moja nilisimama hapa madhabahuni nikiwa peke yangu, lakini nikasema ipo siku nimitasimama na mke wangu madhabahuni. Ninamshukuru Mungu na leo hii Bwana ametupa kibali cha kusimama madhabahuni. Mke wangu alikuwa akiumwa kwa kipindi kirefu na tuliweza kumsafirisha India kwa matibabu na huko waliweza kumfanyia upasuaji wa mgongo. Ilikuwa ni kazi ngumu, tulipita kwenye mambo magumu. Kuna wakati nilimpigia simu Askofu wangu Dkt. Gertrude Rwakatare kumwambia, ninaanza kujifunza jinsi gani Israel walivyolia kwa Musa wakati wamefika kwenye bahari ya Shamu; waliondoka kwa ushindi na kumsifu Musa huku wakienda, wakiimba na kushangilia Musa; lakini wamlipofika kwenye bahari na nyuma wanaangalia kuna jeshi linawafuata, wakalia kilio na wakasahau kuwa ndio wao walikuwa wakimsifu Musa. 
Nami nilimwambia mama Gertrude Rwakatare ninaomba unikumbuke kwenye maombi kwani mimi na mke wangu tulikuwa tunapitia hali ngumu. Lakini ninamshukuru Mungu, Neno likanijiia, na Bwana akanikumbusha katika kitabu cha Yeremia 32:27, Mungu mwenyewe akanikumbusha akisema hivi, “Mimi ni Bwana Mungu wa wote wenye mwili" Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nampigia simu mchungaji wangu Noah Lukumay, na Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare usiku ili tuombe pamoja , na wao walikuwa tayari kutuombea. Leo hii tumesimama hapa kusema, “Yesu ni Bwana na hakuna jambo asiloweza”. Ninachotakata kusema tena ni kwamba, “Mungu anabaki kuwa Mungu na anabaki na nguvu zake na uweza wake”. 
Tumemuona Bwana akitutea. Lakini adui aliendelea kutufuatilia, nakumbuka tulirudi nyumbani Tanzania tukitokea India na mke wangu, mke wangu alipoingia ndani alitereza ndani na akadondoka, sikuweza kuona ile “impact” ya kuanguka kwake, nilidhani ni ile kuanguka kwa kawaida kumbe kulikuwa kuna madhara makubwa. Baada ya siku tatu, nne hivi nikaona joto limebadirika sana na kuwa kama moto katika mwili wake. Lakini nilipooangalia mgongoni kwake sehemu ya mshono (alipofanyiwa upasuaji) nikaona uvimbe umeanza tena, basi nikamchukua mke wangu na kumpeleka katika hospitali ya Moi na Dkt. Sanjoni alipomuangalia vyuma vya X-ray akaona viko sawa, lakini kuna shida katika mwili wake. 
Daktaria akamchoma sindano na alipoivuta ile sindano ikawa imejaa usaha. Kumbe alipondoka chini pale nyumbani vile vyuma vikachoma yake na kukawa na “Internal Paining” na hakuna mahali pa kutokea damu. Lakini Mungu ni mwema, waliweza kumtoa usahau wote na kubaki damu mbichi kabisa na baadae wakatupa “anti-biotic, na sasa ninamshukuru Mungu tupo mahali hapa na anaendelea. Watumishi wa Mungu ninasema hivi, “Yesu alipotoka kwenye maombi ya siku 40 akijaribiwa na shetani, na siku ya tatu alipomaliza, Biblia inasema hivi, shetani alimwacha Yesu kwa muda na baadae aliendelea kumfuatilia. 

Tunamshukuru Mungu ametupa neema ya kulikiri jina lake, kwamba Yesu ndiye njia ya kweli na uzima na ndio maana tunakusanyika kanisani. Lakini usiache kumuomba Mungu kila wakati, kwa maana Mungu ametupa pumzi basi wewe omba. Wiki moja imepita sasa nikiwa kazini, nilipigiwa simu na binti yangu anaitwa Grace akanambia, “Mama sasa hivi haongei, hatikisiki wala hafanyi chochote”, nikasema moyo, “Ile hali ya zamani kumbe bado inaendelea”. Nikamuelekeza binti yangu achuke pesa mahali fulani na apige simu kwa dereva wampeleke hospitalini, na mimi nikaanza safari ya kuwafuata hospitalini. Jamani ule haikuwa ni ugonjwa bali ilikuwa ni vita, na ilikuwa ni roho ya mauti iliyotumwa mke wangu. Pia miguu ya mke wangu ilikuwa inavimba sana, ila Daktari hizi ni “sign effect” za dawa anazotumia. 
Lakini ahimidiwe Yesu ambaye yeye ni Bwana wa vita siku zote kwani alitutetea na kutuvusha na baada ya maombi mke wangu alifunguliwa, na leo amesema, ngoja niende madhabahuni nikapone kabisa. Nami ninamshukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na watumishi wengine wote mliotutumia meseji kwa njia ya simu, nasema, “Mungu awabariki sana”. Hakuna kitu kizuri kama faraja na sio kubeba zawadi. Unakumbuka Yohana alipata kibano, lakini Yesu hakwenda kumtembelea wala kutuma wawakilishi. Yohana alizidi kusikia kuwa Yesu anachapa Injili. Yohana akatuma wanafunzi akasema, “Hivi ni Yeye mwenyewe au tumtazamie mwingine”. Nachotaka kusema ni mwamba, “Mtumishi wa Mungu unapopitia kwenye kibano, usipotezee imani”, ukipita kwenye machungu shika imani”. 
Imani yako ndio itakayokuvusha.

Nami ninamshukuru sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na watumishi wengine wote mliotutumia meseji kwa njia ya simu, nasema, “Mungu awabariki sana”. Hakuna kitu kizuri kama faraja na sio kubeba zawadi. Unakumbuka Yohana alipata kibano, lakini Yesu hakwenda kumtembelea wala kutuma wawakilishi. Yohana alizidi kusikia kuwa Yesu anachapa Injili. Yohana akatuma wanafunzi akasema, “Hivi ni Yeye mwenyewe au tumtazamie mwingine”. Nachotaka kusema ni mwamba, “Mtumishi wa Mungu unapopitia kwenye kibano, usipotezee imani”, ukipita kwenye machungu shika imani”. Imani yako ndio itakayokuvusha.

Nami nimefarajika sana kuona upendo wa Mungu kwa waumini wa kanisa hili la Mlima wa Moto walipomuona mke wangu akiingia kanisani, nao walitoka katika viti vyao na kumkumbatia, nikajisikia faraja, nikajisikia machozi yanataka kunitoka. Sasa ninaomba na mke wangu aseme chochote.

Mke na Mzee Kitalu alikuwa na haya ya kusema, “Bwana Yesu asifiwe, ninamshukuru Mungu sana kwani ameniponya, pia ninamshukuru Mungu kwa kunipa mchungaji ambaye ni mwanamke (Dr. Gertrude Rwakatare) ana roho ya uzazi, Mama Mungu akubariki sana. Ninamshukuru sana Mungu, na walio niombea. Ninafikiri Yule Daktari wangu alikuwa anatumiwa na shetani, tena alimfunga ufahamu, na aliweza kunipa mazoezi siku nne ambayo ni marefu sana, kwahiyo niliporudi nyumbani sikuweza tena kutembea nikaanza kutumia, “wheelchair” na daktari mwingine akanambia, “Sasa Lilian unarudi wodini kwani umeumizwa sana. Ninamshukuru Mungu kwa Mch. Noah Lukumay, nilipokuwa siwezi kutembea bali nimebaki nikilia, aliweza kuniombea na kunifariji. Ninamshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, kwani nilipokuwa nikilia na nikiwa sina mama yangu mzazi nilipokea nguvu za ajabu na faraja. Mungu wangu awabariki sana.