MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

NIDHAMU KATIKA KUTUMIA FEDHA BINAFSI.

Yale mafundisho ya msingi yenye kufungua fahamu bado yanaendelea NCHI YA AHADI kila siku ya Jumapili kuanzia saa tisa alasiri na kuendelea! 
Katika mwendelezo huo Jumapili ya tarehe 10. Feb. 2013 darasa liliendelea na mada iliyokuwa mezani likuwa ni; NIDHAMU KATIKA KUTUMIA FEDHA BINAFSI.
Kimsingi wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa ni kituko fulani pale mtu anapokuwa na fedha (haijalishi ni kiasi gani) halafu hajui namna sahihi ya kuitumia ili kujiongezea kipato. Ni jambo moja kutumia fedha zikaisha lakini pia ni jambo lingine kutumia fedha kuongeza kipato. Ili kutumia fedha uliyonayo kuongeza kipato ni lazima uwe na Nidhamu, Je! Nidhamu hiyo unaipata wapi? Fuata na mtaalamu wa masuala ya Fedha, ndugu JOE BISHOTA ambaye ndie aliyekuwa mzungumzaji siku hiyo. 
Kumbuka, ili upate kila kitu kwa ukamilifu wake, Blog hii inakukaribisha NCHI YA AHADI>>> unaweza kuwasiliana kwa mawasiliano yaliyoandikwa mwishoni kabisa katika somo hili.

NIDHAMU KATIKA KUTUMIA FEDHA BINAFSI (Personal Financial Management).
Na Joe Bishota.

Huhitaji misuli mikubwa kuwa na nidhamu katika fedha yako binafsi, unachohitaji ni kanuni rahisi sana ambazo mtawala wake ni TABIA na UFAHAMU. Tabia inatawala kwa asilimia themanini 80% na Ufahamu unachukua asilimia ishirini 20%.

1. Tabia
Hizi ni tabia ambazo zinakuja kisirisiri kukuchukulia fedha yako bila kujijua. Mfano; mtu mwingine amejiwekea utaratibu kuwa kabla hajaenda kulala usiku ni lazima anywe bia moja au mbili kwa mfano, kimsingi hii ni tabia ambayo inakuchukulia fedha bila kujitambua kwa sababu ukipiga hesabu ya mwezi mzima ni pesa nyingi sana umetumia pasipo ulazima wowote wa kinywaji hicho.

* Kumbuka, utakachokipanda ndicho utakachokivuna.
* Kanuni utakazozipanga maishani mwako ndizo zitakazoamua maisha yako ya usoni (will determine your future).
* Hizi ni kanuni zinazoendesha maisha yetu kimya kimya.
* Asilimia tisini 90% ya matatizo ya fedha tunasababisha sisi wenyewe kwa kutokuwa na mipango thabiti kama sio imara.
* Ni lazima uamue mwenyewe kubadilisha mazingira yako ya fedha.
* Ni lazima ujue nafasi yako (position)
* Lazima ujue thamani yako (value)
* Lazima ujue thamani ya rasilimali zako (assets).

Fanya zoezi la kuorodhesha madeni yako, fanya zoezi la kuandika thamani ya rasilimali ulizo nazo halafu chukua thamani ya rasilimali zako utoe thamani / jumla ya madeni yako; utapata kiasi kinachobaki.
Kama kiasi kilichobaki ni hasi (negative figure) hiyo ndio thamani yako kwa maneno mengine ujue kuwa umefilisika. Kama kiasi kinachobaki ni chanya ujue unaenda vizuri.

* Ukitaka kuendelea katika maisha lazima ujue thamani yako / nafasi yako.
* Mapato yako lazima yazidi matumizi yako, na kile kinachobaki baada ya matumizi ndio utajiri wako. Matumizi yako yakizidi mapato huwezi kutoka kimaisha.

2. Lazima ujue unataka kwenda wapi (Ufahamu).
> Ili kujua unataka kwenda wapi lazima uamue unaanzaje.
> Lazima uendane na wakati / nyakati kuweza kukabiliana na mabadiliko ya ulimwengu / mazingira na nyanja mbali mbali (updates).

KANUNI TANO (5) KATIKA MATUMIZI YA FEDHA BINAFSI.

1. Matumizi Yasizidi Mapato Unayopata.
> Lazima ujue kinachobaki ndio chanzo cha utajiri wako.
> Wekeza kile kinachobaki baada ya matumizi.

2. Lazima Utafute Namna Ya Kuongeza Mapato.
> Unaweza kuanza na vitu vidogo. Watu wengi wanapata promotion kwa sababu tu wanawahi kazini.
> Kuwa smart, usiingie ofisini ukiwa shaghala baghala.
> Jaribu kufanya kitu cha maana katika muda wako wa ziada.
> Kujitolea na kufanya kazi kwa bidii.
> Jenga mahusiano mazuri na watu. Watu wengi wanapenda kufanya kazi na watu wanaoelewana nao. Mahusiano mazuri yatakupa ndisha daraja na kukupa promotion.
> Kwenye mambo ya fedha tabia ndio inayotangulia.
> Kuwa na tabia ya kutaka kuongoza.
> Kuwa tayari kukubali makosa pale unapokosea.
> Usiwe mtu wa kulalamika
> Jifunze kusimamia mambo yako mwenyewe.

3. Jifunze Kuishi Katika Mapato Yako.
mfano. unapoenda kufanya manunuzi (shopping) andika orodha ya vitu unavyoenda kununua (shopping list) na gharama zake. Siku zote unaponunua kitu / vitu omba punguzo (discount).
> Vunja tabia zingine zisizo na manufaa kwako.
> Lazima ujue vitu unavyohitaji na vitu unavyotaka ( hivi ni vitu viwili tofauti).
> Jifunze kununua vitu kwa jumla (wholesale).

4. Lazima ujue namna ya kutunza pesa yako.
Kile kiasi (cash) kinachobaki ndio mlango wako wa kutokea.
Kabla hujalipa madeni, tenga pesa kidogo ya akiba. Ni mwiko kuigusa hiyo pesa ya akiba (emergency fund).
Kabla hujaanza kuwekeza hakikisha tayari una akiba ya dharura.
Haya yote yatakusaidia kujua jinsi ya kushughulika na madeni.

Watu wanaohudhuria darasa la kupanua ufahamu.