RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RAIS AMTEUA MKEWE KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS

Rais wa Nicaragua, Daniel Ortega (70) amemteua mkewe kuwa mgombea mwenza nafasi ya makamu wa rais wakati huu ambapo anawania kuchaguliwa kwa muhula mwingine.

Mkewe Rosario Murillo tayari ana wadhifa maarufu wa msemaji wa serikali, amekuwa akionekana katika runinga ya Nicaragua kila siku na anaonekana kuwa anagawana mamlaka na mumewe.

Wakosoaji wanawashtumu wanandoa hao wawili kwa kuiendesha Nicaragua ambayo inakabiliwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba kama chombo chao cha kibinafsi. Rais Ortega akiwa hazungumzi sana katika vyombo vya habari ,mkewe huonekana mara kwa mara katika runinga akijadili sera na kujikuza .

Akiwa mama wa watoto 7 wa rais huyo anajua kuongea Kiingereza na Kifaransa huku akijulikana pia kuwa mshairi. Pia anasifa za kuvaa mavazi yenye rangi nyingi na vito vya miaka ya sitini.

Wanahabari wanasema kuwa raia wengi wa taifa hilo wanamuona bi Murillo kama mwenye uwezo mkubwa katika taifa lake kutokana na hadhi yake katika uma.

Mume na mkewe waliwasilisha makaratasi yao ya kugombea viti hivyo rasmi katika mji mkuu wa Managua wakiandamana na mshauri wakili wa chama chao cha Sandinista.