MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

SABABU ZA KUVUNJIKA UCHUMBA


1. Kukosa uaminifu katika mahusiano ya uchumba.
mojawapo ya matatizo yanayosababisha chumba nyingi kuvunjika ni suala la kukosa uaminifu na hii hufungulia mlango wa shetani kuwashambulia na hatimaye uchumba kuvunjika na wakati mwingine utawakuta wachumba wakiwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengine na hii husababisha uchumba kuvunjika

2.Roho ya tamaa ya maisha makubwa nje ya uwezo wao.
hali ya kutamani maisha makubwa ambayo nje na uwezo husababisha uchumba kuvunjika na wakati mwingine akijitokeza mtu mwingine ambaye anaonyesha dalili fulani za kuwa na mali au pesa zaidi ya yule mchumba huchangia kuvunjika kwa uchumba hivyo ni vizuri kulidhika na mchumba wako na muanze pamoja na MUNGU atawabarikia mkiwa pamoja.

3.Kujihusisha na tendo la ndoa kabla ya ndoa.
Hili nadhani ni tatizo kubwa labda huenda kuliko haya mengine na hili ni sumu kubwa sana inayovunja chumba za watu wengi, kwanza huondoa imani kwa wale wachumba wenyewe, mtu anawaza huyu kakubali kufanya mapenzi na mimi ipo siku atanichoka na kufanya na mwingine pia kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa huweza kugundua baadhi ya madhaifu na mapungufu aliyonayo mmoja wa wachumba hao na kuamua ikiwa hiki ndicho nakitarajia wakati ndoa mbona nitakuwa nimejitwika tanzi? na hivyo huvunja uchumba na wakati mwingine kuwatangazia watu madhaifu ya mchumba wake.

4.Kuanza kusemasema na kutangaza mapema kabla ya wakati muafaka.
kutangaza juu ya uchumba wenu kabla ya hatua za awali kumesababisha baadhi ya chumba kuvunjika unakuta hatua za awali kabisa kanisa zima wanajua,kila mtaa wanajua yaani kila mtu anajua hii husababisha mmoja ya wachumba kuona kuwa huyu mwenzangu hana siri na hawezi kutunza mambo huenda hata tutakapooana hataweza kutunza siri hivyo anaweza kuvunja uchumba na wakati mwingine kusemasema kabla ya muda huwasababisha wale walio maadui zenu kuwazunguka kwa mbele na kupindua na ghafla unashangaa unakuta yule aliyekua rafiki yako wa karibu uliye kuwa unamshirikisha jambo hilo kakuzunguka na kukugeuzia kibao. Baada ya siku mbili tatu unaskia yuleyule mchumba wako anamvisha pete mchumba wako.

5.Kuwasikiliza watu wengine zaidi ya kumsikiliza MUNGU.
Hii inaweza kusababisha uchumba kuvunjika. ni vizuri kujifunza kumsikiliza MUNGU juu ya yule aliye kuongoza kwamba atafaa kuwa mwenzi wako wa ndoa badala ya kuwasikiliza watu wanasema nini juu ya wewe na mchumba wako. watu wanaweza kumtoa kasoro mfano mchumba mwenyewe hajasoma,ni mbaya,hana figa nzuri,mchafu,hamuendani, maskini na kasoro nyingi tu na hiyo husababisha uchumba kuvunjika

6.Kuchumbiana bila kumhusisha MUNGU.
Mlionana na kuvutiana pasipo kumhusisha MUNGU na kutangaza kwa watu na kuanza mipango ya kuoana ndipo mnakuja kugundua kumbe ilikuwa ni misisimko yenu tu wala MUNGU hakuhusika kabisa katika mchakato mzima wa uchumba wenu na matokeo yake uchumba wenu unavunjika na kuacha ukijiuliza maswali mengi.

7.kutumia muda mwingi katika uchumba kabla ya ndoa.
Kuna baadhi ya wachumba wanatumia muda mwingi sana kukaa katika mahusiano ya uchumba kwa malengo ya kusomana tabia au kuchunguzana au kusubiriana katika masomo nk. Hali hii hupelekea kuchokana katika mahusiano na kuwasababishia kuona kama huenda labda nilichagua mtu asiye sahihi. Baada ya kusoma na madhaifu mengi kwa muda mrefu mwisho uchumba huweza kuvunjika.

8.Roho ya haraka na kukosa uvumilivu.
Wengine wakichumbiana hupeleka mambo haraka haraka utadhani ni dharula, wengi huwa na hali ya kutokujiamini huenda kutokana na yaliyowapata siku za nyuma. labda walichumbiana na baada ya muda mfupi uchumba ukavunjika na kuacha majeraha makubwa hivyo hudhani hali hiyo itajirudia, katika kufanya mambo haraka huweza kusababisha hata huu uchumba kuvunjika.

9.Upinzani wa shetani ili ukose kilicho bora zaidi.
Kuvunjika kwa uchumba wakati mwingine kunaweza kusababishwa na ibilisi shetani ambaye ni mdau wa kwanza wa upinzani juu ya mafanikio ya wana wa MUNGU. Ndiyo maana tunahitaji sana kufunga na kuomba ili kuvunja na kuharibu kazi za shetani na mipango aanayotuwazia sisi katika maisha yetu.

10.Uchumba kuvunjika kwa sababu ya mapenzi ya MUNGU.
Sio kila kitu kinaweza kusababishwa na shetani, wakati mwingine MUNGU mwenyewe huingilia kati na kusababisha uchumba fulani kuvunjika kutokana na sababu za kimungu ambazo wakati mwingine kwetu sisi sio rahisi kuweza kuzijua kwa haraka mpaka wakati kamili wa MUNGU utimie au kusudi lake kujidhihirisha wazi. Ni vizuri kwetu sisi kama watu wa MUNGU kutafuta mapenzi ya MUNGU na kujua kwamba kuna wakati MUNGU mwanyewe anaweza kusababisha uchumba kuvunjika kwa ajili ya usalama wetu.

– kumbuka NDOA SAHIHI NI YA MKE MMOJA NA MME MMOJA {MWANZO 2:24}
– pia NI DHAMBI KWA WACHUMBA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA
– shetani ALIWADANGANYA ADAMU NA EVA KWA SABABU HAPENDI MAFANIKIO KWA WANA WA MUNGU na hata huwadanganya wachumba wengi ili watende dhambi kabla ya ndoa ili maisha yao ya ndoa yasiwe na baraka na pia ndoa hiyo haitakuwa na ulinzi wa MUNGU jambo ambalo ni hatari.
-MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kama hujampatia YESU KRISTO maisha yako unatakiwa ufanye hivyo leo maana pasipo yeye hakuna uzima wa milele (Yohana 14:6) na ukimshirikisha yeye hata kwenye uchumba wako yeye ni ngome imara na atakushindia yote.
-MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula