RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: SHIGONGO: HIZI NDIZO MBINU ZA KUFANIKIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akifundisha wanasemina waliohudhuria somo hilo.


Na Denis Mtima, RISASI Mchanganyiko

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, Jumapili iliyopita alizitaja mbinu za kufanikiwa katika kipindi kigumu, wakati wa semina maalum iliyofanyika katika Ukumbi wa Victoria Christian Centre, Mbezi Beach jijini hapa.
Shigongo akizungumza na wanasemina mara baada ya kumaliza kuwafundisha.

Alisema kuwa katika kipindi kigumu cha uchumi, kuna watu wanatengeneza utajiri, wengine wakifilisika, baadhi yao wakifukuzwa kazi na wapo wanaopandishwa vyeo.
“Mambo makuu ya kuzingatia katika kipindi kigumu ni kutoingiwa na hofu, kulichambua tatizo, kubadilika kuendana na wakati na kuwa na msimamo au lengo lako,” alisema.

Alizitaja mbinu zingine kuwa ni ubunifu zaidi wa biashara, kujiwekea tabia njema na kuwa mbunifu wa kutengeneza vyanzo vingi vya mapato vinavyoendana na wakati huo.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria somo hilo.


Mbinu nyingine ambayo Shigongo alisema itamsaidia mtu kukipita vizuri kipindi kigumu ni kuhifadhi na kununua bidhaa nyingi zinazokuwa zikiuzwa na watu, kuhakikisha anaongeza matangazo ya shughuli anazozifanya ili watu watazame bidhaa zake, kuweka uhusiano wake karibu na Mungu ili amsaidie kwa atakavyo.
Vilevile aliyatolea ufafanuzi yote aliyowafundisha jinsi yanavyoweza kumsaidia mtu katika kipindi kigumu cha uchumi na kukabiliana na hali hiyo ya maisha.
Aidha, kipengele cha kuhifadhi na kununua bidhaa nyingi, alisema mtu anachotakiwa kufanya ili biashara yake iimarike ni kununua bidhaa zinazouzwa kwa kipindi hicho na watu wengine, mfano nyumba ambazo zinakuwa zinauzwa kwa bei ya chini ambapo baadaye wakati uchumi ukiimarika, mtu anaweza kuziuza na kupata faida zaidi.


Semina Kubwa ya Eric Shigongo Ilivyowafungua Akili Vijana: Part 1