RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

21.08.2016: WATU WAZIDI KUOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI-HIZI NI PICHA ZA WALIOKOKA

Watu wazidi kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao. Siku ya Jumapili 21.08.2016 watu wengi walijitokeza katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuombewa na kuongozwa sala ya toba. Watu walimkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Uamuzi waliochukua ni uamuzi sahihi kwa maana hapa duniani sisi ni watu wa kupita na makao yetu yako mbinguni.

Mungu ameweka siri kubwa sana kwa wanadamu ya kutambua ni lini unaweza kufa. Watu wangejua kifo chao wangefanya mambo yao kwa kujiamini na wakijua siku ikikaribia ya kifo chao wataokoka. Lakini tunatakiwa kutambua kuwa hatujui ni lini tutaiagaa hii dunia yenye mvuto ukiingalia kwa macho

Watu wengi wanateseka sana na maisha haya kwasababu shetani anawatumikisha na kuwatesa bila ya wao kutambua. Ni vyema ukatambua kuwa mateso unayopata ni kazi ya shetani, na kuepukana nayo ni kuokoka tu na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kama Biblia inavyosema.

Mungu amemuweka mtumishi wake Mama wa Upendo Dr. Bishop Rwakatare kuwa balozi wake wa hapa duniani, amemteua kwa kazi yake ya kuwatangazia watu habari njema ili siku ya mwisho wakamuone Mungu. Ni vyema kama utakuwa msikivu pale anapokuambia jambo la kufanya ili kukuimarisha katika zoezi zima la IMANI yako na Mungu. Bishop anatumika kama bomba la kupitisha ujumbe wa Mungu kwako.

Tuna kila sababu ya kuwashukuru watumishi wa Mungu, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Otieno na Mch. Francis Mahichi waliongoza sala ya toba kwa hawa ndugu zetu walioamua kuokoka na baadae kupelekwa kubatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumanne walianza masomo ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Ni wajibu wako na mimi kuwaombea hawa ndugu zetu ili wadumu katika wokovu. Tunakuaribisha na wewe kanisani ili tuabudu pamoja. Mungu akubariki sana. Ibada zetu kwa siku ya Jumapili zinaanza saa 3 asubuhi. Usafiri ni bure kutoka katika kituo cha masi cha Makumbusho au Kituo cha Mwenge kwenye mataa, utaon magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B"












 Mch. Otieno akitoa Neno kabla ya kuombewa na kubatizwa

 Mzee wa kanisa Mzee Malya akiwaombea
 Mch. Otieno akiongoza sala ya Toba
 Mch. Prisca Charles akiwaombea