MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

15.09.2016: MUUNGWANA BLOG: MREMA AMPONGEZA RWAKATARE KUTOA WAFUNGWA

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema

Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amempongeza Mchungaji Getrude Rwakatare kwa kwa kubeba gharama ya Sh 25 milioni kuwalipia faini wafungwa 78 na kuwawezesha kurudi uraiani kuungana na ndugu zao.

Mrema pia ametumia nafasi hiyo kumuomba Rwakatare kuratibu harambee kwa ajili ya kukusanya fedha za kugharamia kuwatoa wafungwa wenye Parole kwa kuwa Serikali imeelemewa na haina fedha hizo hali ambayo imewafanya waendelee kusota magerezani badala ya kuungana na familia zao kama nguvu kazi.

Rwakatare mwenyewe amesema anafurahi kwa sababu nemo la Mungu lilimkumbusha kuwajali wafungwa, ingawa kwa muda mrefu wachungaji akiwamo na yeye wamekuwa wakijihusisha katika kuwahudumia na kuwasaidia yatima, wajane na walemavu huku wafungwa wakisahaulika.

CHANZO CHA HABARI: http://www.muungwana.co.tz/2016/09/mrema-ampongeza-rwakatare-kutoa-wafungwa.html