Select Menu

News

IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JUMAPILI HII

MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JUMAPILI HII

MTUME DR. PETER NYAGA

MTUME DR. PETER NYAGA

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» » ASKOFU WA ENGLAND AJITANGAZA KUWA SHOGA


Sanga Rulea 3:02 PM 0


Askofu Nicholas Chamberlain.

Askofu mmoja wa Kanisa la Kianglikana nchini Uingereza amekuwa wa kwanza kutangaza hadharani kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja na sasa yuko kwenye uhusiano.

Askofu huyo aitwaye, Nicholas Chamberlain, amesema kuwa walioshiriki katika mchakato wa kumteua mwaka uliopita walielewa fika mwelekeo wake wa jinsia.

”Watu wanajua nashiriki mapenzi ya jinsia moja, lakini si kitu cha kwanza nachoweza kumwambia yeyote. Jinsia ni sehemu ya yule niliye, lakini ni kazi yangu ya kitume ambayo ninataka kuiangazia .”

Nicholas Chamberlain anasema hata hivyo anafuata kanuni za kanisa zinazosema kuwa haruhusiwi kuoa.

Msemaji wa Kanisa la England amesema: “Nicholas hajamkera yeyote na amekua wazi na mkweli ukiuliza. Suala lake si la siri, ingawa ni la kibinafsi kama ilivyo kwa wale walio katika mahusiano ya kimapenzi .”

Inadhaniwa kuwa hakuna askofu yeyote anayehudumu aliyewahi kutangaza hadharani msimamo wake wa kingono.

Kanisa la Kianglikana kote duniani limegawanyika sana miaka ya hivi karibuni kuhusu masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia na kutawazwa kwa makasisi walio katika mapenzi ya jinsia moja.

Credit: BBC

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS