MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE NA JOPO LA WACHUNGAJI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAKIMUOMBEA MH. DKT. AUGUSTINO MREMA KATIKA OFISI YA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE

Siku ya leo Alhamisi 15.09.2016 "Super Woman" kama watu wanavyombatiza jina hili kupitia facebook, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa na wachungaji wa Mlima wa Moto na waandishi wa habari aliweza kumuombea afya njema na kazi yake ya kulijenga Taifa.

Mh. Dr. Augustino Lyatonga Mrema alifika kanisani hapo kwaajili ya kumpongeza Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuwatoa wafungua 78 gerezani kwa kuwalipia faini ya Tsh. Mil. 25

Tunamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha "Super Woman" (kama wadau walivyo,pa jina hilo) Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuchukua hatua ya busara na yenye hekima kumuombea kiongozi mkubwa wa serikali.

Tuna kila sababu nasi kumuombea Mh. Dkt. Augustino Mrema ili azidi kufanya kazi yake ya kulijenga Taifa la Tanzania. Tunakumbuka katika viongozi waliotikisa na kuhamasisha Ukristo miaka iliyopita alikuwa ni Mh. Dkt. Augustino Mrema, nasi leo tuna kila sababu ya kumpongeza na hasa kumuombea yeye na familia yake.

Endelea kufuatilia post zetu kujua ujio wa Mheshimiwa huyu kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"